Vigezo 13 vilivyowekwa na CCM
katika Uchaguzi Mkuu wa 2005 kumpima mwanachama anayefaa kugombea urais,
ndivyo vitakavyotumika kuwaengua makada wanaoendelea kujitokeza kuwania
nafasi hiyo mwakani, imefahamika.
Vigezo hivyo vinaonekana kuwa kizingiti kwa baadhi
ya makada wa chama hicho ambao tayari wametangaza na wengine wanaotajwa
kutaka nafasi hiyo ya juu nchini, ukiachilia mbali mnyukano
unaotarajiwa kutoka vyama vya upinzani vinavyoonekana kupata nguvu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula
amelithibitishia gazeti hili kwamba, “Sifa hizo 13 zilizotumika mwaka
2005 na 2010 ndizo zitakazotumika pia mwaka 2015 na wala hakutakuwa na
maboresho wala nyongeza ya aina yoyote.”
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Vigezo hivyo viliwekwa ili kuhakikisha chama hicho
kinampata mgombea asiyetiliwa shaka juu ya vitendo vya uadilifu, mwenye
uzoefu wa uongozi serikalini, atakayedumisha muungano, mwenye upeo wa
masuala ya kimataifa, mtetezi wa wanyonge, asiyejilimbikizia mali na
mwajibikaji, mambo ambayo hata hivyo, bado yameibua mjadala iwapo
yanazingatiwa au la.
Pia anayetakiwa lazima awe mwenye kuzitetea sera
za CCM, anayekubalika na wananchi, asiye na hulka ya udikteta au
ufashisti, mwenye uwezo wa kufanya uamuzi wa busara na kiwango cha elimu
ya chuo kikuu au inayolingana nayo.
Licha ya vigezo hivyo, baadhi ya makada
waliokwishajitokeza na wengine wanaotajwa wanaonekana dhahiri kukosa
baadhi sifa hizo na wengine wako ‘kifungoni’ kwa miezi 12 baada ya
kupewa onyo kali kwa kufanya kampeni mapema na kujihusisha na vitendo
vinavyokiuka maadili ndani ya chama na jamii.
Vigogo wa CCM ambao wanatajwa kutaka kupewa ridhaa
ya kupeperusha bendera ya chama hicho ambao iwapo watachukua fomu,
watatazamwa kwa vigezo hivyo ni Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla,
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January
Makamba ambao wamekwishatangaza kuwania nafasi hiyo.
Wengine ambao wanatajwa ingawa hawajatangaza nia
hadharani ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa; Waziri Mkuu mstaafu,
Frederick Sumaye; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa;
Bernard Membe; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu);
Stephen Wasira na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William
Ngeleja.
Wachambuzi wanavyosema
Akizungumzia vigezo hivyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu
cha Tumaini, Danford Kitwana alisema CCM inajua kuwa hakuna mgombea
anayeweza kuwa na sifa zote 13, kwa hiyo inapaswa iangalie ni nani
anawazidi wengine.
“Kigezo cha kuwa na sifa ya maadili ndicho
kinachowakwamisha wengi, pia hakuna mgombea anayeweza kuwa na sifa zote
zilizowekwa na chama, mwingine anaweza kuwa na sifa saba, nne au tano.
“Wakitumia mfumo wa kuwatazama wagombea wao kwa idadi ya sifa, mtu mwenye sifa nyingi ndiye asimamishwe kugombea.”
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Mwananchi
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk Emmanuel Mallya
alisema Tanzania inahitaji kuongozwa na rais mwenye historia ya uadilifu
wa matumizi ya fedha za umma.
“Tunahitaji kiongozi anayeweza kusimamia fedha za
umma, si mtu anayenunua vitu ovyo bila kujali Hazina kuna kiasi gani,
hilo ni tatizo kubwa,” alisema Dk Mallya.
Aliongeza kuwa, kiongozi huyo lazima awe
mchapakazi anayeweza kuwaletea wananchi maendeleo, lakini watu wengi
wamekuwa wakisema wanamtaka mtu mwadilifu bila kuzungumzia uwezo wake wa
kufanya kazi.
Mwalimu mstaafu wa shule ya msingi, Rehema Mathayo
alisema kutokana na baadhi ya viongozi ndani ya CCM kukumbwa na kashfa
za ufisadi, anayetaka kugombea urais lazima awe ‘msafi’ ndani na nje ya
chama.
“Mshindi ndani ya chama ni mtu atakayekuwa
amewashinda wenzake kwa kuwa na maadili mazuri na asiwe na doa lolote la
kujishughulisha na ‘dili’ za ajabu,” alisema Rehema.
Mwalimu huyo aliongeza kuwa mgombea huyo lazima
awe na uzoefu mkubwa wa masuala la kimataifa kwa kuwa hata kama atakuwa
na maadili, kama hafahamu namna ya kuwaunganisha wananchi na jumuiya za
kimataifa, hatakuwa na manufaa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Ernest
Mwasalwiba alisema kutokana na kuporomoka kwa maadili hususan kwa
viongozi wa umma, vitendo vya rushwa na kadhia mbalimbali, rais ajaye
anatakiwa kuhakikisha yale anayoyasema ndiyo anayatenda na Watanzania
hawahitaji Rais dikteta.
“Masuala ya maadili, rushwa, yote haya yanazuiwa
mpaka sasa lakini suala ni usimamizi tu... ni wakati sasa wa rais ajaye
kuonyesha ajenda yake itakuwa ipi, anapokuwa amesema kitu kila mtu
lazima afuate mfano akisema anachukia rushwa na maadili kwa yaheshimiwe
isiwe ni mjadala kila mtu anafuata kuanzia chini hadi juu.
“Dikteta siyo kiongozi tunayemtaka, bali tunataka
kiongozi atakayesimamia sheria na mifumo iliyopo iweze kufanya kazi
ipasavyo... mfano Rais Jakaya Kikwete kipindi anaingia aliingia na
kaulimbiu ya ‘Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya’ ambayo ilifuatwa hadi
na viongozi wa halmashauri.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Romanus
Dimoso alisema: “Sifa za rais huwa zinajulikana. Tunahitaji rais ajaye
anayejua hali ya kisiasa ilivyo kwa sasa, hatutaki rais ambaye hatambui
mchango unaotolewa na vyama vingi vya siasa na jinsi atakavyoweza
kufanya navyo kazi hususan kwa kuhakikisha demokrasia inazingatiwa.”
Aliongeza: “Je, malengo ya anayetaka urais yale ya
kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 nchi hii inafikia uchumi wa kati.
Amejipanga vipi kama mtumishi wa kwanza wa Taifa hili kutufikisha
huko?... Hatutaki mtu awe rais tu kwa jina.”
Rais mstaafu wa Chama cha Madaktari Tanzania
(MAT), Dk Primus Saidia alisema: “Tunahitaji rais anayeweza kufanya
uamuzi mgumu kwa mustakabali wa Taifa, asiwe rais wa maneno maneno, bali
wa vitendo. Anasema dawa hospitalini hakuna na kesho zinakuwapo.
“Tunataka mtu mwenye historia ya uongozi, ameshawahi kufanya nini katika
kuboresha sekta ya afya, elimu, uchumi na kijamii? Alishafanya maamuzi
magumu yapi ambayo kila mmoja aliyaona na aliyaheshimu?”Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment