Askofu Telesphor Mkude wa Kanisa
Katoliki Jimbo la Morogoro
WATUMISHI wa umma wa ngazi mbalimbali waliopewa dhamana ya
kuwatumikia wananchi wameombwa kuzisoma na kusikiliza kwa umakini hotuba
mbalimbali za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili
ziwaweke kwenye msingi wa kuwa na maadili mema, uadilifu na uwazi.
Changamoto hiyo imetolewa na Askofu Telesphor Mkude wa Kanisa
Katoliki Jimbo la Morogoro, hivi karibuni wakati akizungumza na gazeti
hili kwenye ofisi ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrice, mjini Morogoro.
Akijikita katika suala la maadili ya viongozi wa umma, Askofu Mkude,
alisema suala la kufuata maadili, kuonesha uadilifu na uwazi katika
uwajibikaji wa kuwatumikia wananchi ni sifa kuu ya kiongozi yoyote yule.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Askofu Mkude alisema ni muhimu kwa viongozi wetu wakazirejea hotuba
mbalimbali za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ambaye wakati wa utawala
sifa kuu ya kiongozi ilikuwa ni mwonekano wake katika maadili na
uzingatiaji wa miiko ya uongozi.
“Nadhani kuna mahali tumeteleza ...viongozi wetu wengi hawatendi
majukumu yao kwa kufuata maadili, uadilifu na uwazi na hili ndilo
lililotufikisha hapa tulipo...ni budi tukaangalia wapi tulikotoka na
tunaelekea wapi ili tujisahihishe,” alisema Askofu Mkude.
Hivyo alisema, Mwalimu Nyerere alilijenga taifa la watu wenye kuwa na
uzalendo wa nchi yao na viongozi walioteuliwa ama kuajiriwa kuwa
watumishi wa umma walifuata maadili ya utumishi wao tofauti na iliyo
sasa.
“ Mwalimu Nyerere alikuwa mwadilifu katika matendo yake
…hakujilimbikizia mali na hata watoto wake walikuwa ni sawa na watoto wa
watu wa kawaida...na ndiyo maana alikuwa na uwezo wa kukemea maovu na
wakosaji wakatii,“ alielezea:
“ ...Mwalimu Nyerere alijenga tabia ya kufuatilia nyendo za viongozi
wake na pale alipoona ama kubaini kiongozi wake anakwenda kinyume na
utaratibu hakusita kumuita ofisini na kumkanya sambamba na kumwongoza
njia nzuri, “ alibainisha Askofu Mkude.
Hivyo alisema, kutokana na misimamo hiyo iliyotokana na uadilifu
wake, hotuba zake alizokuwa akizitoa miaka mingi ya nyuma zinaporudiwa
kwenye redio ama televisheni, zimekuwa na mvuto na mafunzo ndani yake
kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Kwa mujibu wa Askofu huyo, hivyo ni vyema viongozi wa sasa pamoja na
kuwa na majukumu mengine ya kikazi, ni jambo jema pia wakajikumbusha kwa
kuzisikiliza kwa makini na zinaweza kuwarejesha kwenye mstari wa kuwa
waadilifu, wanaofuata maadili mema ya utumishi wa umma na kujenga zana
ya uwazi na uwajibikaji katika jamii.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Habari Leo
No comments:
Post a Comment