Wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15.
Shambulizi
hilo lilitokea katika kijiji cha Kautikari katika jimbo la Borno, pale
washukiwa wa Boko Haram walipowasili kijijini humo kwa magari yenye
silaha, wakilenga askari wa ulinzi wa jadi wa mji huo.Kijiji hicho kipo karibu na Chibok mahali ambapo kundi la Boko Haram, liliwateka nyara wasichana wa shule zaidi ya mia mbili mwezi Aprili mwaka huu.
Zaidi ya watu elfu kumi wameuwawa Nchini Nigeria na Boko Haram mwaka huu pekee. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment