SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeahirisha mechi za raundi ya
tisa na kumi za timu nne zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na
kuziruhusu kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza
kesho hadi Januari 13, 2015 Zanzibar.
Timu za Tanzania bara zitakazoshiriki ni mabingwa watetezi Azam FC, Simba, Yanga na Mtibwa Sugar.
Awali, kabla ya TFF kushindwa kuthibitishiwa uwepo wa mashindano hayo
kutokana na viongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kupelekana
mahakamani, timu zilikuwa zikiendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi za
raundi ya tisa zilizokuwa zifanyike Jumamosi ijayo.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Akizungumza jana Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum alisema kesi
iliyokuwa ikiwakabili imekwishaondolewa mahakamani na mashindano
yataendelea kama yalivyopangwa.
“Maandalizi yanakwenda vizuri na timu zitaanza kwenda Zanzibar
kuanzia kesho (leo) ambapo ni Simba na KCCA za Uganda itafika kesho
asubuhi(leo asubuhi),” alisema.
Timu nyingine zinazotarajiwa kushiriki kwenye michuano hiyo mabingwa
wa Zanzibar KMKM, Police FC, JKU, Mtende Rangers na Shaba FC wakati za
kigeni ni El Merreikh ya Sudan, Ulinzi Kenya na mabingwa wa kombe hilo
KCCA.
Alisema wamekuwa wakichagua timu ambazo ni kubwa na zenye mashabiki
wengi Zanzibar ili mchezo kuwa na msisimko na wenye kuvutia. Alitaja
zawadi kuwa mshindi wa kwanza ataondoka na Sh milioni 10 na wa pili Sh
milioni tano.
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura alisema kutokana na
michuano hiyo ya Mapinduzi, timu hizo za Tanzania zitalazimika kucheza
mechi za Ligi katikati ya wiki baada ya kumaliza michuano hiyo.
Hii itakuwa ni mara ya tisa kufanyika kwa michuano hiyo tangu
ianzishwe kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12, 1964. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment