Wednesday, December 31, 2014

RAIS MPYA WA TUNISIA KUAPISHWA

Rais mteule Beji Caid Essebsi kuapishwa kama rais mpya wa Tunisia baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Tunisia 
 
Rais mteule wa Tunisia Beji Caid Essebsi anatarajiwa kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza uliokuwa huru nchini humo. Alimshinda rais aliyekuwa mamlakani Moncef Marzouk. Ushindi wake unaaminisha kwamba Tunisia ndilo taifa ambalo limejinasua kutoka utawala wa kiimla hadi ule wa kidemokrasia.
Siku ya jumatatu,tume ya uchaguzi ilithibitisha kuwa bwana Essebsi alishinda kura ya raundi ya pili dhidi ya Marzouk. Rais huye mteule ataapishwa katika bunge la wawakilishi wapwa ambapo chama chake Nidaa Tounes kimepata wabunge wengi.
Raia wa Tunisia wakisherehekea ushindi wa Caid Essebsi
Tayari maandalizi ya kumuapisha yamekamilika mjini Tunis.
Hatua hiyo hiyo itafikisha tamati mvutano wa demokrasia wa miaka minne ya ghasia zilizoghubika taifa hilo zilizopeleekea kung'olewa kwa utawala wa Rais Zine el-Abedine Ben Ali.
Bwana Essebsi alihudumu katika utawala wa Ben Ali, pamoja na uongozi wa rais wa zamani Habib Bourguiba. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...