Wednesday, December 31, 2014

RAIS JAMMEH "BADO NIPO MADALAKANI"

Rais wa Gambia Yahya Jammeh 
 
Rais wa Gambia amesema kuwa bado analiongoza taifa hilo la Afrika magharibi baada ya vikosi vyake vya usalama kutibua jaribio la mapinduzi.
Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.
Hatahivyo hajulikani aliko.Milio mikali ya riasi ilizuka karibu na makao ya rais katika mji mkuu.
Bwana Jammeh alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka 1994 na wapinzani wake wamekuwa wakimkosoa kwa uongozi wake wa kiimla.
Duru za kidiplomasia na zile za kijeshi zinasema kuwa wanajeshi kutoka kwa jeshi la ulinzi wa rais wanadaiwa kufanya shambulizi hilo katika makao ya rais mjini Banjul mapema siku ya jummane.
Serikali imekana kwamba kulikuwa na jaribio la mapinduzi katika taarifa iliotangazwa katika radio ya taifa.
Hatahivyo,bwana Jammeh baadaye alikiri kuhusu shambulizi hilo na kusema kuwa wanajeshi waaminifu wa Lamin Sanneh aliyemtaja kama mwenye aibu walivamia mji mkuu wa Gambia kutoka Senegal katika jaribio la kutaka kuipindua serikali yake.
Amesema kuwa wavamizi hao hatahivyo walikabiliwa na vikosi vya usalama na kuwaua wanne kati yao huku wengine wanne zaidi wakikamatwa. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...