Wednesday, December 31, 2014

MZUNGU WA SIMBA AMETUA ASUBUHI HII KUMRITHI PHIRI


IMG-20141231-WA0000
KOCHA mpya wa Simba sc, Mserbia Goran Kapunovic amewasili asubuhi ya leo majira ya saa 1:00 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Goran ametua kwa ndege ya Shirika la Qatar Airways na baada ya kuwasili amesema amekuja kufanya kazi na sivinginevyo.
Hata hivyo kocha huyo anayerithi mikoba ya Patrick Phiri amesema atazungumza mengi baada ya kumalizana na viongozi na kuanza kazi yake.
Goran anatarajia kuiongoza Simba kwa mara ya kwanza katika mechi za kombe la Mapinduzi linaloanza kutimua vumbi kesho januari mosi mwakani. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...