Monday, December 29, 2014

MGOMBEA URAIS ATABIRIWA KIFO

 
Maalim Hassan Hussein (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaama jana.

Maalim Hassan Hussein, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, marehemu Sheikh Yahya Hussein, ametabiri mambo 18 yatakayotokea mwakani, likiwamo la kufariki ghafla kwa kiongozi mmoja mzee ambaye yumo kwenye mbio za urais mwakani.

Hussein alisema jana kuwa kiongozi huyo atadondoka ghafla kwenye jukwaa na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali. Akitangaza utabiri wa mwakani, alisema: “Kiongozi huyo atakufa wakati akipelekwa hospitalini.”

Alisema pia mwandishi mmoja mashuhuri nchini atakufa kifo chenye utata kitakachoitesa Serikali na familia yake katika kutafuta sababu za kifo chake. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Mtabiri huyo alisema nyota inaonyesha kwamba misiba miwili ya kitaifa itatokea mwakani.

Kuhusu uchaguzi wa kiti cha urais mwaka 2015, alisema kati ya kundi la vijana na wazee, nyota zinaonyesha kwamba watakaofaidika ni vijana.

“Lakini kuna wazee pia wanaoweza kufaidika, hawa ni wale wenye sura za ujana, yaani babyface au wenye kupenda mambo ya ujana na kushirikiana na vijana,” alisema.

Alisema ili Tanzania ilinde sifa ya kuwa nchi yenye amani na utulivu ni kuwa na Rais kijana mwenye mchanganyiko wa dini mbili au mwenye ndoa ya dini tofauti.

Alisema utabiri unaonyesha kuwa mwaka 2015 utatawaliwa na nyota yenye kupendelea vijana, hivyo ni vyema vyama vya siasa vikawasimamisha kugombea nafasi za urais, ubunge na udiwani.

Kuhusu mauaji, fujo na ghasia alisema vitatawala katika uchaguzi ujao na kwamba Serikali inatakiwa kuweka tahadhari kubwa.

Pia alitabiri viongozi wawili wa siasa na dini kukumbwa na kashfa ya ngono itakayowasababisha anguko la utumishi wa kutukuka na familia zao.

Alisema mwaka ujao utakuwa na mafuriko na dhoruba vitakavyosababisha madhara, hivyo tahadhari ichukuliwe kuanzia sasa.

Alisema kutakuwa na vifo vya ghafla vya wasanii, wanamichezo na watu maarufu kama ilivyokuwa mwaka 2014.
Maalim Hussein alisema lile tishio la wahisani kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi, litalegezwa na kuifanya nchi kuingia katika Uchaguzi Mkuu kwa staha.
Alisema wazee wataendelea kushutumiana na kupingana hadharani, hali itakayosababisha migawanyiko ndani ya vyama vya siasa na nchi kwa jumla.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...