Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu
MBIO za urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimechukua sura mpya
baada ya jana Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kutangaza
rasmi nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka kesho.
Nyalandu anaungana na makada wengine wa CCM wakiwemo mawaziri
waandamizi katika serikali ya Rais Kikwete, mawaziri wakuu wastaafu na
hata wabunge waliotangaza nia au kutajwatajwa kwa nafasi hiyo, hivyo
kuongeza joto la urais ndani ya CCM.
Akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru wapiga kura wake kwenye
uwanja wa michezo wa Shule ya Msingi Ilongero Wilaya ya Singida Vijijini
jana, Nyalandu mmoja wa waziri vijana, alisema muda wa Tanzania kupata
maono mapya umefika.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Muda wa Tanzania kupata maono mapya umefika, nitachukua hatua ya
kuelekea Dodoma kuchukua fomu muda ukifika, maelfu ya watu
watanisindikiza,wanawake, vijana, wanawake kutoka mikoa mbalimbali.
“Naitazama mpya siku ambayo ndoto yangu itakamilika, Mungu atanyanua
vyombo na kushangaza wakubwa. Najua tulikuwa wadogo kama Nazareti,
lakini Ilongero imekuwa na mchango mkubwa ambao utakuwa si faida kwa
wana Singida bali taifa zima la Tanzania,” alisema Waziri Nyalandu.
Alisema kila mtu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais ndani ya CCM, lazima kazi zake zipimwe kwa moto.
“Wale wote waliotangaza nia ndani ya chama chetu, kazi zao lazima
zipimwe kwa moto na zianikwe hadharani ili mwisho wa siku CCM yenyewe
itazipima,”alisema Nyalandu.
Aliongeza kuwa, pindi Rais Jakaya Kikwete atapohitimisha utawala
wake, lazima atakabidhi kijiti kwa kizazi kipya, hivyo ndani ya CCM
anaamini utakuwa mwaka wa mabadiliko na fikra mpya.
“Tuna wajibu wa kubadili fikra zetu,watu wasimamie Tanzania kuchukua
hatua, licha ya ukweli kwamba CCM tuna utaratibu na itikadi
zetu,tumeondoa zuio kwa vijana wasiwe waoga…tumejipanga kuwashangaza
wengi,”alisema Nyalandu.
Wapinzani
Alisema muda wa kuwashangaza wengi unaanzia kwa vyama vya upinzani,
zikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi
(CUF) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
“Katika safari yangu ya miaka ya ubunge, Mungu ametusaidia kusonga
mbele, safari moja huanzisha nyingine, nawaomba tusonge tena kwa hatua
nyingine, mlianzisha safari yangu ya kisiasa nilikuwa kama mzabibu
uliotoa matunda, mkaniita ‘Mwanyengu’ maana yake mtoto wa tai la
kuishangaza dunia.
Safari hii imekuwa ya milima na mabonde kwa pamoja tumeweza, Mungu ameona,Kikwete ameona sawasawa.
“Nikitazama naona nchi hii inahitaji kubadilika kama nyingine
zilizopiga hatua, Rais Kikwete amesimama kama jemedari, shujaa,
mpambanaji hapa alipofika lazima tupapongezee,” alisema Nyalandu.
Alisema anatambua atapitia kwenye ushindani mkubwa ndani ya chama,
ambao utatoa mtu mmoja wa kupeperusha bendera ya chama hicho kugombea
urais wa Tanzania.
“Nawambia wale wote wanaoogopa kushindanishwa ni waoga, siku, saa,
mwezi na hata mwaka utakapofika chini ya Kikwete,wachukue fomu na
kupeleka kazi zao ili zipimwe,” alisema Nyalandu.
Katika mchuano ndani ya CCM, Nyalandu anatarajiwa kuchuana na
wanaotajwatajwa, wakiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mawaziri
waandamizi, Stephen Wasira (Ofisi ya Rais, Uratibu na Mahusiano),
Bernard Membe (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), mawaziri wakuu
wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye na Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Wengine ni wabunge, Dk Hamisi Kigwangalla, William Ngeleja na wengine ambao wanahusishwa, lakini hawajajianika hadharani. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Habari Leo
No comments:
Post a Comment