Monday, December 29, 2014

YANGA NA AZAM ZASHINDWA KUTAMBIANA

 
Hamisi Tambwe na Msuva wakishangilia bao leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Afrika mwakani, Azam na Yanga zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Azam ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofunga na Didier Kavumbagu dakika 6, Yanga walisawazisha kupitia Amiss Tambwe (7) na kupata la pili lililofungwa na Simon Msuva (57), kabla ya John Bocco aliyeingia akitoa benchi alisawazisha Azam dakika 65.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 14, sawa na Azam, wakati Mtibwa Sugar imebaki kileleni ikiwa na pointi 16, baada ya kulazimishwa sare 1-1 na Stand United jana asubuhi mchezo huo juzi ilivunjwa kutokana na mvua kubwa kunyesha.
Mbeya City imejiondoa mkiani baada ya kuichapa Ndanda FC 1-0, wakati Polisi Morogoro imeinyuka Mgambo JKT kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Morogoro: Polisi Morogoro wameutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani kwa kuichapa Mgambo JKT kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Polisi ilipata bao kwanza dakika 22, lililofungwa na Nicolaus Kabipe kabla ya Iman Mapunda kupachika bao la pili kwa kichwa dakika 85, akiunganisha kona ya Kabipe.
Mbeya: Deus Kaseke aliwainua mashabiki wa Mbeya City dakika pili kwa kufunga bao pekee akiunganisha kwa shuti lililomshinda kipa wa Ndanda FC, Salehe Marande na kujaa wavuni. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...