TIMU ya soka ya Mtibwa Sugar ambao ni vinara wa Ligi Kuu Tanzania
bara jana ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Stand United ya Shinyanga
katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro jana
asubuhi.
Mchezo huo ilikuwa uchezwe juzi lakini ulivunjika katika dakika ya
sita baada ya mvua kubwa iliyosababisha maji kujaa kwenye uwanja wa
Manungu na kuamuliwa uchezwe jana saa mbili asubuhi.
Katika mchezo huo wa jana wachezaji wa Stand United walionesha mpira
wa kuvutia hasa kipindi cha kwanza na kuwawezesha kupata bao la kuongoza
katika dakika ya 22 ya mchezo.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Bao hilo lilipachikwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Shaaban Kondo
baada ya kuunganisha krosi ya Haruna Chanogo. Baada ya kuingia bao hilo
Mtibwa Sugar ilikianza kipindi cha pili kwa mashambulizi makali langoni
mwa Stand United, lakini kikwazo kikubwa alikuwa kipa Mohamed Makaka kwa
kuokoa mikwaju mingi ya hatari ya washambuliaji wa timu ya Mtibwa
Sugar.
Juhudi za Mtibwa kusaka bao la kusawazisha zilizaa matunda katika
dakika ya 86 baada ya Said Mkopi kufunga kwa kichwa. Mkopi aliliokoa
jahazi la timu yake lisizame baada ya kutumia vyema mpira wa kona na
iliyochongwa na Jamal Mnyate .
Wakati huo huo, katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri
Morogoro jana jioni Polisi ya mjini hapa iliibuka na ushindi wa mabao
2-0 dhidi ya Mgambo JKT ya Tanga.
Polisi ilianza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 22 mfungaji
akiwa Nicolas Kabipe aliyefunga kwa shuti kali baada ya kuunganisha pasi
ya Said Bahanuzi kabla ya kumbabatiza kipa wa Mgambo, Said Lubawa.
Imani Mapunda aliifungia Polisi bao la pili kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona iliyopigwa na Kabipe.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment