
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema vijiji
45 mkoani Mara vinatarajiwa kuunganishiwa na huduma ya umeme kupitia
Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Alisema hayo katika ziara yake ya siku sita katika mkoa wa Mara,
lengo likiwa ni kukagua na kuzindua miradi ya umeme vijijini
inayosimamiwa na REA awamu ya pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme
Nchini (Tanesco).
Alisema ziara yake iliyohusisha wilaya za Musoma, Tarime, Rorya,
Bunda na Serengeti, ililenga kubaini na kukagua mahitaji ya umeme katika
wilaya hizo ili vijiji vilivyokosa umeme kwenye awamu ya pili,
viingizwe katika awamu nyingine ya umeme vijijini.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.













Wagonjwa wakimtia adabu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Nyakabale
mkoani Geita, Josephat Msafiri baada ya kuwatelekeza juzi.










