Thursday, December 25, 2014

KESI YA MH. NASSARI YAAHIRISHWA

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari  

Kesi ya kuchoma moto bendera ya CCM inayomkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari jana iliahirishwa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Maji ya Chai, Ndikilo Mbise kutokana na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Maji ya Chai, David Mwita kuwa safarini.
Akiahirisha kesi hiyo, Mbise alisema itatajwa tena Januari 20 mwakani.Mbise alisema Hakimu Mwita amepata msiba, hivyo amekwenda nyumbani kwao mkoani Mara huku, hakimu mwingine wa mahakama hiyo akiwa likizo.
Mbise alisema ameahirisha kesi na kuipangia tarehe nyingine kwa kuwa ni mlinzi wa amani wa eneo hio.
Katika kesi hiyo, Nassari ambaye hakuhudhuria mahakamani hapo kutokana na kuwa safarini, anatuhumiwa kuchoma bendera ya CCM Desemba 15, saa 11 jioni katika eneo la Maji ya Chai. Bendera hiyo yenye thamani ya Sh250,000 ilikuwa mali ya Raphael Moses.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa ataendelea kuwa nje kwa dhamana ya wadhamini watatu ya Sh1.5 milioni kila mmoja. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...