Thursday, December 25, 2014

PLUIJM NA PHIRI WAJIGAMBA

Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm




Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm na mwenzake Patrick Phiri wa Simba wametamba kuibuka na ushindi dhidi ya Azam na Kagera Sugar wakati mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zitakapoingia raundi ya nane kuanzia kesho.

Pluijm alisema kuwa anaiheshimu Azam FC kama moja ya timu bora kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, lakini hana hofu yoyote.

“Nawaandaa vyema vijana wangu waibuke na ushindi kwenye pambalo hilo kwa sababu litatuweka kwenye nafasi nzuri nje na ndani ya uwanja,” alisema Pluij
m. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pluijm aliongeza kuwa moja ya mkakati wake hivi sasa ni kuhakikisha kuwa kila mchezaji wa kikosi hicho anakuwa fiti kwa asilimia mia moja, ili kuwa na kikosi kikubwa kwa ajili ya mashindano ya ndani pamoja na ya kimataifa.

“Nataka wote wawe fiti na pia kila mchezaji nitampa nafasi ili niwe na wigo mpana wa uteuzi wa wachezaji wa kikosi cha kwanza kuliko kuwa na kikosi kidogo ambacho kinaweza kukugharimu pale timu inapopata majeruhi au mchezaji fulani anapokosekana.”

Naye Phiri alisema kwa kujiamini kuwa sasa matokeo ya sare yatabaki historia katika kikosi chake kutokana na usajili mzuri waliofanya.

Simba ambayo katika mechi saba za raundi ya kwanza ilipata sare sita na kushinda moja, kesho itakuwa na kibarua kizito mbele ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mwendelezo wa Ligi Kuu.

Kikosi chote cha Simba kilikuwa kambini Zanzibar isipokuwa mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi ambaye imeelezwa kuwa yupo jijini Dar es Salaam akitokea Uganda ambako alikwenda kufunga ndoa.

Waganda wengine beki Juuko Murshid na winga Simon Sserunkuma walijiunga na kambi hiyo juzi na kuanza mazoezi na wenzao.

Phiri alisema anaamini timu yake itafanya vizuri na kusahau yaliyopita katika kuhakikisha wanamaliza katika nafasi tatu za juu. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...