Thursday, December 25, 2014

CHENGE, NGELEJA KUADHIBIWA NDANI YA SIKU 21 ZIJAZO

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti bungeni, Andrew Chenge


Wenyeviti watatu wa Kamati za Bunge waliopendekezwa kuwajibishwa na Bunge hilo katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow wataondolewa katika nyadhifa zao ndani ya siku 21 zijazo, imeelezwa.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema jana kuwa utekelezaji wa maazimio ya Bunge kwa upande wa mhimili huo wa dola utafanyiwa kazi mapema mwakani.

“Hilo litatekelezwa wakati wa Kamati za Bunge ambazo zitaanza mwishoni mwa wiki ya pili ya Januari mwakani kwa kamati husika kuchagua wenyeviti wapya.”

Wenyeviti hao ni wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, William Ngeleja wa Katiba, Sheria na Utawala na Andrew Chenge wa Kamati ya Bajeti. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Tuhuma zao

Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi (CCM) alitajwa katika ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa aliwekewa Sh1.6 bilioni katika akaunti yake binafsi kama ilivyokuwa kwa Ngejela (Sengerema -CCM) ambaye aliingiziwa Sh40.4 milioni. Wote waliingiziwa fedha hizo na mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering & Marketing, James Rugemalira.

Mwambalaswa, ambaye pia ni Mbunge wa Lupa (CCM), ametajwa kwa kuwa alikuwa makamu mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco ambayo Bunge liliazimia kuwa wajumbe wake wawajibishwe.

Katika azimio namba tatu, Bunge lilielekeza kuwa kamati husika za kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao wenyeviti tajwa wa kamati husika za kudumu za Bunge.

Utekelezaji wa azimio hilo unakuja baada ya Serikali kuanza kuwawajibisha vigogo wake waliotajwa katika ripoti hiyo.

Jumatatu iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alimfukuza kazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye kama ilivyokuwa kwa Chenge na Ngeleja, aliingiziwa Sh1.6 bilioni katika akaunti yake binafsi kinyume na kanuni za maadili ya viongozi wa umma.

Pia, wakati Rais Kikwete akimuweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, juzi Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alimsimamisha kazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

Hao wote walitanguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ambaye alijiuzulu kutokana na kashfa hiyo akisema ushauri wake haukueleweka hivyo kuchafua hali ya hewa. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...