Thursday, December 25, 2014

MAXIMO "MKAKATI WANGU UMENIONDOA YANGA"




Kocha Marcio Maximo 


Kocha Marcio Maximo amesema hana kinyongo na uamuzi wa uongozi wa Yanga kumuondoa, ingawa umefuta ghafla mkakati wa kutaka klabu hiyo iendeshwa kwa weledi.

Maximo na msaidizi wake Leonard Neiva walisitishiwa mikataba yao baada ya Yanga kufungwa na Simba 2-0 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe mwezi huu, ikiwa ni takriban miezi mitano tangu aje nchini.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupanda ndege kurudi kwao Brazil jana, Maximo alisema hana kinyongo na uamuzi huo, lakini akaitaka klabu hiyo kongwe kuendeleza soka la vijana na kutengeneza mindombinu kama inataka kupata mafanikio makubwa katika soka.

Alisema katika muda mfupi aliokuwa klabu hiyo, alijenga misingi ya utendaji kazi wa kisasa ndani na nje ya uwanja kwa wachezaji ili waweze kujitambua katika kazi yao, lakini jambo hilo limeishia njiani. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.



“Katika miezi sita niliyokuwa na timu, nilijaribu kujenga weledi ndani na nje ya uwanja, tulifanya kazi kubwa ya kujaribu kutengeneza miundombinu, lakini tulishindwa kuwashawishi viongozi wote,” alisema Maximo ambaye timu yake ililazimika kuhama viwanja kwa ajili ya mazoezi kutokana na Uwanja wa Kaunda kuwa katika hali mbaya.

Yanga bado inapambana na mamlaka za jiji ikidai iongezewe eneo ili ijenge uwanja wa kisasa, maombi ambayo yamekataliwa na hivyo timu kulazimika kukodi viwanja tofauti kwa ajili ya mazoezi.

“Hii inatokana na ukweli kuwa baadhi ya viongozi hawakupenda yale tuliyokuwa tunayafanya. Labda sisi hatukuwa makocha wa aina yao ndio maana walichukua uamuzi waliouchukua. Hatuna kinyongo hata kidogo. Tutakuwa sehemu ya timu hiyo na pale watakapotaka ushauri wetu tutakuwa tayari kutoa,” alisema kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa.

Alisema uamuzi uliochukuliwa ni kawaida kwa kuwa ni sehemu ya changamoto katika maisha ya ukocha pamoja.

“Ili kupata kazi ya ukocha, lazima kutakuwa na tukio la kufukuza kocha. Kuondoka kwetu sisi kuna watu wengine wameingia. Maisha bado yanaendelea. Si ajabu kwani kuna ushahidi kuwa baadhi ya makocha walikatishiwa mikataba yao na kurejea tena katika timu hiyo hiyo, kama ilivyotokea kwa Jose Mourinho, aliondoka Chelsea na kurejea tena kutokana na uongozi kutambua kile alichokuwa anakifanya kabla hajasitishiwa mkataba wake,” alisema.

Maximo anaondoka akiwa ameiacha Yanga katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...