Thursday, December 25, 2014

VIJIJI 45 KUPATA UMEME MARA

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema vijiji 45 mkoani Mara vinatarajiwa kuunganishiwa na huduma ya umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Alisema hayo katika ziara yake ya siku sita katika mkoa wa Mara, lengo likiwa ni kukagua na kuzindua miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na REA awamu ya pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco).
Alisema ziara yake iliyohusisha wilaya za Musoma, Tarime, Rorya, Bunda na Serengeti, ililenga kubaini na kukagua mahitaji ya umeme katika wilaya hizo ili vijiji vilivyokosa umeme kwenye awamu ya pili, viingizwe katika awamu nyingine ya umeme vijijini. 
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Alieleza kuwa Wizara imekuwa ikisambaza umeme katika kila Mkoa na Wilaya za Tanzania kwa awamu, kulingana na mahitaji na idadi ya watu katika maeneo hayo.
Alisema kwa sasa umeme unaosambazwa upo katika awamu ya pili, ambapo awamu ya tatu itakuja baada awamu ya pili kumalizika.
Alisema vipaumbele vinavyotolewa katika uunganishaji wa umeme vijijini ni maeneo yenye huduma muhimu za kijamii kama shule, vituo vya afya, makanisa, misikiti, ofisi za vijiji na kata na sehemu zenye miradi ya maji.
“Lengo letu kuu kwanza ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za jamii kwa urahisi na baada ya kuboreshwa kwa huduma hizo tunakwenda kuwaunganishia umeme wananchi mmoja mmoja, ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha maisha ya wananchi yanaboreshwa kupitia nishati ya umeme,” alisema Muhongo
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...