Viongozi wa UKAWA
VYAMA vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),
vimetaka sheria ya maadili itungwe upya ili kuweka uwazi wa watu wote
kuona taarifa ya mali za viongozi.
Vyama hivyo vinaamini hatua hiyo, itasaidia wananchi wote kujua mali
halisi za viongozi na pia itasaidia kupunguza ufisadi, kutokana na
wananchi kutambua ukweli wa mali za viongozi wao.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa umoja huo, Profesa Ibrahim Lipumba
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana
kuhusu hatua zinazostahili kuchukuliwa, kutokana na suala la uchotwaji
wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.