Wednesday, March 13, 2013

Mchakato wa kumpata Papa mpya huko Vatican bado hakijaeleweka makadinali leo waingia siku ya pili ya kupiga kura.


Moshi mweusi ulifuka jana jioni kutoka kwenye  dohani huko Vatican ikiwa ni ishara kwamba Baraza la siri la Makadinali bado halijampata Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki baada ya kupiga kura ya kwanza.
Mchakato wa kupiga kura ulianza mapema jana  ambapo Makadinali 115 kutoka nchi 48 walikutana kwa faragha ili kumchagua atakaechukua nafasi ya aliyekuwa papa Benedikt wa 16 aliejiuzulu mwishoni mwa mwezi uliopita.
Zoezi la kupiga kura litaendelea hadi hapo mmoja wa Makadinali atakapopigiwa theluthi mbili ya kura yaani kura 77.
Atakaefikia kiwango hicho atakuwa Baba Mtakatifu wa 266.
Ikiwa Makadinali, wanaopiga kura watakubaliana juu ya Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki, moshi  mweupe utatoka dohani na kengele zitapigwa kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican. 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...