Wednesday, March 13, 2013

Mama Salma Kikwete akitaka kituo cha utamaduni cha Bujora kuhifadhi utamaduni wa mtanzania.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekipongeza kituo cha utamaduni cha Bujora kwa kutunza na kuhifadhi  utamaduni wa mtanzania unaolitambulisha kabila la wasukuma jambo litakalosaidia kizazi kijacho kuweza kujifunza utamaduni huo.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo (WAMA) ametoa pongezi hizo hivi karibuni alipokitembelea kituo hicho kilichopo wilayani Magu katika mkoa wa Mwanza.
Amesema kuwa kituo hicho kimeonyesha mfano wa kuigwa kwani amejionea na kujifunza mambo mbalimbali ambayo hakuwa anayafahamu hapo awali kuhusiana na kabila hilo jambo la muhimu wahakikishe kuwa wanaendelea kutunza utamaduni wao.
Akisoma taarifa ya kituo hicho Padre Fabian Mhoja ambaye ni Mkurugezi amesema kuwa kituo kilianza mwaka 1954  kikiwa na lengo la kuhifadhi na kuendeleza tunu bora ya maisha ya watu ili waweze kumfahamu Mungu na kuishi kadiri ya mpango wake kwa kutumia utamaduni.
Amesema kuwa wanajihusisha  na shughuli za kutunza  na kuendeleza urithi wa utamaduni wa mtanzania kwani kupitia kituo hicho wameweza kutangaza utalii na utamaduni ndani na nje ya nchi kupitia ngoma , nyimbo na michezo mbalimbali.
Kituo hicho kimekuwa kikiandaa tamasha la Bulabo ambapo Rais Dk. Jakaya  Mrisho Kikwete amekuwa akichangia ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka na kukusanya watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...