Waziri
wa Wizara ya Utalii na Utamaduni wa Zambia Mh. Sylvia Masebo kipokea
zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce
Nzuki Mara baada ya kutembelea katika banda la Tanzania na kukutana na
viongozi Kadhaa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na kufanya nao
mazungumzo kuhusiano na ushirikiano kati ya Zambia na Tanzania katika
masuala ya Utalii Bodi ya Utalii Tanzania inaongoza ujumbe wa
Wafanyabiashara ya Utalii zaidi ya 43 kutoka nchini Tanzania katika
maonyesho ya dunia ya (ITB) yanayofanyika kwenye jengo la Mense Berlin
jijini Berlin UjerumaniWaziri
wa Wizara ya Utalii na Utamaduni wa Zambia Mh. Sylvia
Masebo akisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya
Maliasili na Utalii Bw. Ibrahim Mussa akizungmuza wakati waziri huyo
alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya (ITB) jijini Baerlin
jana katikati ni Katikati ni Balozi Chiti Balozi wa Zambia nchini
Ujerumani
Friday, March 08, 2013
HII NDIO TAARIFA YA ALIEUWAWA NA SIMBA AKIWA KWENYE TENDO LA NDOA
Mashuhuda wanasema wakati mwanamke huyo akishambuliwa na Simba, boyfriend wake alifanikiwa kukimbia akiwa uchi huku akiwa bado amevaa kinga (Condom)
Mwanaume huyo alikimbia kuomba msaada akiwa mtupu bila nguo lakini wengi hawakumuamini wakijua ana upungufu wa akili.
Baadae ndio watu walimuamini na
kumsindikiza polisi alikopewa msaada wa polisi na askari wa Wanyama
pori Zimbabwe na kuelekea mpaka kwenye eneo la tukio ambako ilifyetuliwa
risasi moja na kukuta mwanamke ameshafariki tayari huku akiwa
ametapakaa damu mwili mzima na kujeruhiwa vibaya mwilini ikiwemo
shingoni ambapo waumini wa kanisa moja karibu na hapo walitoa ushuhuda
wa kuona Simba 7 kwenye eneo la tukio. Wakati huohuo mwili wa mwanaume mmoja ambae hakutambulika kirahisi ulikutwa akiwa ameshafariki karibu na ZESA social club huku My Zimbabwe wakiripoti mwanaume huyo kushambuliwa na Simba muda mfupi uliopita. Tukio jingine liliripotiwa kwamba mwanaume aitwae Musinje pia alishambuliwa na Simba na kufariki dunia wakati akitoka kwenye club ya usiku ambapo mwili wake ndio uligundulika baadae ambapo Wakazi wa Kariba wanasema ni watu watatu wameuwawa na Simba kwenye eneo hilo ndani ya saa 24. |
Vigogo wavuliwa madaraka TBS
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), imewavua madaraka wakurugenzi wawili.
Mwenyekiti
wa Bodi hiyo, Profesa Cuthbert Mhilu alisema jana kuwa waliovuliwa
madaraka ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora, Dominic Mwakangale
na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upimaji na Huduma za Vifungashio, Kezia
Mbwambo.
Profesa
Mhilu alisema hatua hiyo imekuja baada ya bodi hiyo kufanya usaili kwa
vigogo mbalimbali wa shirika hilo ulioanza juzi asubuhi hadi saa 3:00
usiku.
Katika
taarifa hiyo, Profesa Mhilu ambaye hakutaka kuingia kwa ndani juu ya
hatua hiyo, alisema viongozi hao watapangiwa kazi nyingine.
“Kwa
kipindi kirefu, TBS imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali
yaliyochangia kudhoofisha utendaji wa watumishi na kulifanya shirika
kukosa tija na ufanisi. Bodi imeonelea ikae mara moja kuchambua,
kujadili na hatimaye kufikia uamuzi wenye lengo la kuweka mazingira bora
na kuwezesha kuanza utatuzi wa matatizo ili shirika lifikie malengo
yake.”
HII NDIO DAWA YA WEZI: SIKU HIZI HAKUNA KUWAUWA NI ADHABU KAMA KAWA:
MWIZI WA BETRI YA GARI ANAEJULIKANA KWA JINA MOJA TU SEFA AKISURUBIWA KWA STAILI YA AINA YAKE KWA KUFUNGWA KWENYE NGAZI PAMOJA NA BETRI ALIYOIBA |
MWIZI HUYO AKIENDELEA KUTESEKA KATIKA NGAZI HIYO |
POLISI WAMEFIKA KUMWOKOA MWIZI HUYO KATIKA MATESO HAYO |
BADO WANANCHI WANAHASIRA NA MWIZI WAO WAKIDAI WAACHIWE WAMFUNZE ADABU MAANA AMEWASUMBUA SANA ENEO HILO LA UYOLE |
POLISI WAMEZIDIWA WAMEPOKONYWA MTUHUMIWA WAO KIPIGO KINAENDELEA |
IPO HAJA YA KUJIFUNZA KUTOKA FINLAND- MASELE
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini, Mhe.
Stephen Masele, akimuonesha Balozi wa Finland nchini,Sinikka Antila
ramani ya maeneo ambapo kuna madini na uchimbaji unaendelea.
Serikali
imesema inahitaji kujifunza zaidi kutoka Finland hususan katika
uchimbaji wa madini ili kuwa na uchimbaji wenye tija kwa taifa.Hayo
yalisemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Stephen Masele
alipokutana na Balozi wa Finland nchini, Sinikka Antila.Masele alisema
Tanzania inahitaji kujifunza masuala ya uchimbaji madini kutoka Finland
kwa kuwa mazingira ya uwekezaji ya nchini humo yanashabihiana na
mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania.“Unajua kampuni kubwa
zinazojishughulisha na uchimbaji madini nchini Finland siyo za hapo
Finland bali ni kampuni kutoka nchi nyingine yani multi-nationals na
hili pia ndilo linalofanyika hapa kwetu Tanzania” alisema.
Mhe. Sophia
Simba ( Mb) akichangia ajenda kuhusu Utokomezaji na Umalizaji wa
Unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike wakati wa mkutano wa 57
wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Wanawake (CSW). Mkutano huu wa
wiki mbili unaendelea hapa Umoja wa Mataifa na Mhe. Simba anaongoza
ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliyeketi nyuma ya Mhe.
Waziri ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Mwinyi
Makatibu
Wakuu, Kijakazi Mtengwa ( Tanzania Bara) na Fatma Gharib Bilal (
Zanzibar ) wakifuatilia majadiliano kuhusu utokomezaji na umalizaji
unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike.
Mhe. Sophia
Simba akishiriki majadiliano ya mada iliyohusu umuhimu wa Takwimu
katika kushughulikia unyanyasaji wa kijinsia, Waziri alikuwa mmoja wa
wazungumzaji wakuu katika mjadala huo. mjadala ulikuwa umeandaliwa na
UNFPA, ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 57 wa CSW,kulia kwa Waziri ni Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA, Bi Anne -Brigitte Albractsen.
Kutokana na
wingi wa washiriki wa majadiliano kuhusu umuhimu wa Takwimu katika
kushughulikia unyanyasaji kuwa wengi kupitia uwezo wa ukumbi, baadhi ya
washiriki walilazimika kukaa chini kama inavyoonekana katika picha
Ziara ya Rais wa Zanzibar Mkoa wa Mjini
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,
akisalimiana na Mwakilishi wa Kiembesamaki Mansoor Yussuf Himid,
alipowasili katika viwanja vya Pwani ya Mazizini kuzindua Soko la
Samaki.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe kushoto akimuonesha picha
za maeneo yaliotoswa matumbae ya kutengeneza, wakati Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika
ziara ya kutembelea Maendeleo ya Mkoa wa Mjini Magharibi.
Wavuvi wa
Dago la Mazizini Pwani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia
baada ya kuwafungulia Soko lao la Samaki, lililojengwa kwa nguvu za
Wananchi na Mradi wa Tasaf Unguja.
Boti za
Patro za Idara ya Uvuvi Zanzibar ambazo hutumika katika kufanyia doria
katika bahari ya Zanzibar kupambana na Wavuvi haramu wanaoharibu
mazingira ya baharini.
Thursday, March 07, 2013
TATOO YAMPONZA MONALISA
SIRI
ya kuvunjika kwa ndoa ya staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry ‘Monalisa’
imevuja ambapo imeelezwa kuwa tattoo aliyokuwa ameichora mkononi mwake
yenye alama ya kopa na mshale ndiyo chanzo.
Akizungumza na Tollywood Newz jijini
Dar es Salaam, Monalisa alisema: “Sikuwahi kuwaza hili hata mara moja.
Siku moja Kanisani, Mchungaji aliniambia kwamba tattoo yangu ndiyo
chanzo cha kunivurugia uhusiano wangu.
“Aliniambia kwamba, alama ya
kopa ambayo humaanisha moyo – upendo, halafu mshale kupita katikati
yake, humaanisha maumivu na kuteswa katika uhusiano. Lilikuwa jambo
jipya kwangu lakini niliamua kufuta haraka sana na sasa nimeweka
nyingine ya ua rose.”Source:Globalpublishers
Prof. Maghembe alichefua kanisa
WAZIRI wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe,
amelaumiwa na uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa kwa kushindwa
kuingilia kati mgogoro wa maji uliopo kati ya mwekezaji wa mashamba ya
mpunga Mbarali na Shule ya Sekondari ya Kilimo ya Montfort ambayo
inauziwa
maji ili kuweza kulima.
Kuibuliwa
kwa tuhuma hizo zilizoelekezwa moja kwa moja kwa Waziri Maghembe
kunafuatia barua kadhaa zilizoandikwa kwenda wizarani na uongozi wa
kanisa hilo na ule wa shule hiyo pasipo kujibiwa na serikali licha ya
uwekezaji wa kanisa ulilenga zaidi kuwaendeleza vijana.
“Bado
tunaumizwa sana na suala la maji, tumeipigia sana magoti serikali ili
itusaidie tupate maji ya kutosha. Shule yetu ni ya mchepuo wa kilimo,
ilisajiliwa tukijua kuwa tutalima kwa vitendo baada ya kujiridhisha kuwa
maji yapo, tangu apewe mwekezaji ameamua kutuuzia maji,” alilalamika
Mkuu wa Shule hiyo, Ansgar Kigane.
Kigane
alisema kuwa tangu shule hiyo ilipoanzishwa miaka 25 sasa imefanya
vizuri sana kwenye masomo ya kilimo kutokana na upatikanaji wa maji
uliokuwa ukitolewa na Shirika la Kilimo na Chakula (NAFCO) kabla ya
kubinafsishwa.
“Kwa
kuwa shule yetu ni ya kilimo hasa mpunga na kwa kuwa wanafunzi waliweza
kulima na kupata mavuno ya kutosha ilikuwa rahisi kwao kupata chakula
bure shuleni, sasa hali imekuwa ngumu, mwaka huu imebidi tununue maji
kutoka kwa mwekezaji kwa masharti magumu,” alisema.
Alibainisha
kuwa licha ya jitihada kubwa za kuiomba Wizara ya Maji iingilie kati
ili kuona uwezekano wa shule hiyo kupata maji kwa kupitia mfereji mdogo
ulioruhusiwa wakati wa NAFCO, lakini wamekosa majibu sahihi.
Ofisa
Maji Mkuu wa Bonde la Rufiji ambao ndio wenye mamlaka ya kusimamia maji
katika Bonde la Usangu, Idrissa Msuya alisema kwa mujibu wa sheria ya
maji, mwekezaji aliyepewa kibali cha kuyatumia haruhusiwi kuyauza na
kwamba makubaliano yaliyofikiwa ni uamuzi wa pande mbili ambazo
haziihusu mamlaka hiyo.
Msuya
alisema kuwa mvutano huo wa maji umefumuka baada ya serikali
kubinafsisha mashamba ya NAFCO kwani huko nyuma hali haikuwa hivyo na
kwamba mamlaka hiyo imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuleta suluhu ila
anashangaa kwanini hawakubaliani.
Askofu
wa Jimbo Katoliki la Iringa, Tarcisius Ngalalekumtwa, katika barua zake
amekuwa akifanya jitihada kubwa za kuipigia magoti serikali ili iweze
kuiruhusu shule hiyo ipewe kibali cha kutumia maji kutoka kwenye mfereji
wa umma uliojengwa na serikali.
SOURCE::TANZANIA DAIMA::
SNURA ANASWA NA NJEMBA
POZI
la staa wa sinema Bongo, Snura Mushi na Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
kama walivyonaswa na kamera ya Tollywood Newz linatoa ishara kwamba ni
wapenzi.
Fukuafukua
za kitaani zinaeleza kuwa wawili hao ni wapenzi lakini Snura anafanya
siri ili mpenzi wake huyo asiporwe na wajanja.Snura alipoulizwa uhusiano
wake na Dj huyo alisema: “Jamani Ommy ni mtu wangu wa karibu...kama ni
suala la picha, napiga na watu wangapi jamani? Kwa nini iwe kwa Ommy
tu?”
BARUA YA MWANAFUNZI ALIEMALIZA FORM 4 2012 KWA WIZARA YA ELIMU
Pliz my name is MKUWA RAJAB I
am finish fom for. Ze everybody is to say we get za divishen 0, My part I am
saying not I am not get divshen 0. I am vere vere intelijens, but pipoz don’t
like me.
I have experience in singing bongoflava, so pipoz are jelas, the have put ...majik so I get diveshen 0. But I am clever becoz ask me forekzampo, what is fomula for water? Ze fomula for water iz Hech to O.
Now why you give me dishen 0? Ok ask me anadha forekzampo what iz President of America? Ze president of America iz Obama. Ze gavament shud change my marks to dishen 2, because the youth are ze future of my country.
If we get divishen 0 zen all the future is divishen 0. So giv us more maks becoz of ze future. Pliz mzee put on ze yua fb wall so ze Plezident will see.......
Kwa
mantiki hii, tatizo la kushuka kwa kiwango cha elimu nchini
kimesababishwa na wanafunzi wenyewe? Au Wazazi? Ama Waalimu? au mitaala
ya kufundishia? Piga kura yako upande wa kulia kwenye poll vote side
.... Tutabaini tatizo lipo wapi. ....
Kwa hisani ya James Pricenn
Brighton
WAUGUZI MOROGORO WAPOKEZANA KUWASHIKIA DRIPU WAGONJWA BAADA YA KUKOSA VITANDA
BAADHI
ya wananchi wa mkoani MOROGORO wameshangaza na kitendo cha waunguzi
wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro,kupokezana kuwashika madripu ya
dawa wagonjwa waliolaza chini ya wodi za hospital hiyo ya rufaa nya
mkoa wa Morogoro baada ya kukosa vitanda.
.
Skendo zinazidi kuiandama hospital
hiyo ambayo imepandishwa hadhi ya kuwa hospital ya rufaa hivi karibuni
ambapo ljumaa iliyopita mtangazaji wa Top redio ya mkoani hapa Edward
Abed Mganga aliyevamiwa na majambazi na kukimwizwa kwenye hospital hiyo
imeilalamikia hospital hiyo kwakumtelekeza bila kumpa huduma kwa zaidi
ya masaa matano na kuladhimika kuondoka kwenye hospital hiyo ya serikali
na kwenda kutibiwa hospital za watu binafsi.
Mtandao huu umeibua Skendo
nyingine ndani ya hospital hiyo baada ya kushuhudia waunguzi wa hospital
hiyo wakipokeza kuwashikia madripu ya dawa wagonjwa waliolazwa chini
ya sakafu baada ya hospital hiyo kukosa wodi na vitanda vya kutosha.
Juzikati
hospital hiyo ilivamiwa na majeruhi zaidi ya 60 waliopoteza fahamu
baada ya kiwanda cha kutengeza nguo za michezo cha Mazava kukumbwa na
shoti ya umeme na kukimbizwa kwenye hospital hiyo,hivyo uongozi wa
hospital hiyo baada ya kuelemewa na wingi wa majeruhi hao ulilazimia
kutoa magodoro stoo na kuwalaza chini baadhi ya majeruhi hao kufuatia
hospital hiyo kukosa wodi na vitanda vya kutosha.
" Hii ni aibu kubwa kwa hospitali ya
rufaa ya mkoa kuwalaza chini wagonjwa hata kama wakijitetea kwamba
wagonjwa wamekuja kwa mkupo. hospital inapopewa hadhi ya rufaa inamaana
inamudu kukabiliana na majanga yoyote kwa maana wa kuhudumua majeruhi
zaidi ya mia watakaofika kwa mkupuo kwenye hospital hiyo"alisema Bi Asha
Abdallah aliyekuwepo ndani ya wodi namba 3 walipolazwa majeruhi hao.
Vile vile mwandishi wa matandao
huu mbali ya kushudia wauguzi hao wakipokezana kuwashikia madripu
wagonjwa hao pia walishuhudia wahudumu hao wakilazimika kupita juu ya
wagonjwa waliolazwa kwenye eneo la njia za wodi hizo
Ili kupata ufafanuzi wa jambo
hilo Mtandao huu ulimsaka Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo kwa zaidi ya
siku tano na kufanikiwa kumpata leo asubuhi ambapo alipotakiwa kueleza
hali hiyo Mganga huyo mfawidhi Bi Rita Lyamuya alikuwa na haya ya
kusema
" Nikweli siku ile ya tukio la
kiwanda cha Mazava tulitoa magodolo stoo na kuwatandikia chini baadhi ya
majeruhi .kiukweli kwa ishu kama ile tulikosa namna ya kukabiliana
nayo kwani walikuja kwa mkupua zaidi ya majeruhi 65 hivyo tulichofanya
tuliwapokea na baadhi kuwalaza chini na kuwapatia hudumu ya kwanza huku
tukitafuta sehemu muafaka ya kuwalaza"alisema Dr Rita
dustanshekidele blog
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ITALAZYA WILAYANI MBEYA VIJIJINI WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKANA NA UKOSEFU WA VYOO
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ITALAZYA WAKIWA DARASANI HUKU DAWATI MOJA WAKIWA WAMEKALIA WANAFUNZI WATANO |
HII NDIYO HALI HALISI YA VYOO HIVYO KWAKWELI NI HATARI KABISA VIPI WAHUSIKA MPOOO NA MNALIONA HILI? |
HIVI NI VYOO VYA WAALIMU WA SHULE HIYO |
WANAFUNZI SASA HUJISAIDIA KATIKA VICHAKA HIVI KWAKWELI HATARI SANA KUKUTANA NA NYOKA NA WADUDU WENYE SUMU KALI |
PICHA NA KAMANGA MBEYA |
CHADEMA WAZUA GHASIA MAZISHI YA MOLLEL
Wafuasi wa Chadema, wameibua tafrani ya
aina yake wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja
wa Vijana wa CCM (UVCCM), marehemu Benson Mollel baada ya kung’oa
bendera za chama hicho na kuamsha hasira za
waombolezaji wafuasi wa chama tawala.
Mollel
alikutwa amefariki mwanzoni mwa wiki, katika Hoteli ya Lush Garden
Business, Mtaa wa Jacaranda Arusha huku mwili wake ukiwa mtupu.Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana na baadhi ya makada wa CCM
walionekana wakiwasaka wafuasi hao wa Chadema.
Mashuhuda
walisema tukio hilo lilitokea saa 8:30 usiku na baadhi ya wafuasi
wanaosadikika kutoka Chadema walichukizwa na kuwapo kwa bendera hizo
msibani na hivyo kuanza kuzing’oa.
Subscribe to:
Posts (Atom)