Friday, March 08, 2013


Mhe. Sophia Simba ( Mb) akichangia ajenda kuhusu Utokomezaji na Umalizaji wa Unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike wakati wa mkutano wa 57 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Wanawake (CSW). Mkutano huu wa wiki mbili unaendelea hapa Umoja wa Mataifa na Mhe. Simba anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliyeketi nyuma ya Mhe. Waziri ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Mwinyi
Makatibu Wakuu, Kijakazi Mtengwa ( Tanzania Bara) na Fatma Gharib Bilal ( Zanzibar ) wakifuatilia majadiliano kuhusu utokomezaji na umalizaji unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike.
Mhe. Sophia Simba akishiriki majadiliano ya mada iliyohusu umuhimu wa Takwimu katika kushughulikia unyanyasaji wa kijinsia, Waziri alikuwa mmoja wa wazungumzaji wakuu katika mjadala huo. mjadala ulikuwa umeandaliwa na UNFPA, ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 57 wa CSW,kulia kwa Waziri ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA, Bi Anne -Brigitte Albractsen.
Kutokana na wingi wa washiriki wa majadiliano kuhusu umuhimu wa Takwimu katika kushughulikia unyanyasaji kuwa wengi kupitia uwezo wa ukumbi, baadhi ya washiriki walilazimika kukaa chini kama inavyoonekana katika picha

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...