Monday, March 16, 2015

WAHAMIAJI 64 KUTOKA ETHIOPIA WAKAMATWA

Ramani ya Tanzania
Polisi mkoa wa Dodoma nchini Tanzania wanawashikilia wahamiaji haram 64 raia wa Ethiopia, huku mmoja wao akipatikana akiwa amekufa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amenukuliwa akisema wanamshikilia dereva wa gari lililokuwa limewabeba watu hao ambao inaaminika walikuwa njiani kuelekea kusini mwa Afrika.
Hii si mara ya kwanza kwa wahamiaji wa aina hiyo kukamatwa katika mazingira hayo.
Mwaka 2012 watu 42 kutoka Eritrea walikutwa wamekufa katika lori mkoa wa Dodoma kwa kile kinachosemekana ni kukosa hewa kutokana na kufichwa ndani ya lori hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAMILIONI WAANDAMANA BRAZIL

Rais Dilma Roussef wa Brazil
Zaidi ya watu milioni moja kutoka nchini Brazil wameandamana dhidi ya rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff, huku wengi wao wakitaka rais huyo afunguliwe mashtaka ya ufisadi mkubwa uliofanyika katika shirika la mafuta la serikali, Petrobras.
Maandamano kama hayo yamefanyika katika miji mingi ya Brazil ikiwemo mji mkuu wa nchi hiyo Brasilia.
Maandamano makubwa kabisa yamefanyika katika mji wa Sao Paulo ambalo ni eneo la upinzani waliokuwa wakipita mitaani.
Mmoja wa waandamanaji Francisco Pestana alilalama akisema"Dilma hana uwezo wa kuongoza nchi yetu. Tunachokabiliwa nacho ni bahati mbaya sana, namna mamabo yanavyokwenda, yanaweza kuelekea kubaya zaidi, tutakuwa Venezuela nyingine."
Naye mwandamanaji mwingine mwanamke Janaina Lima anasema "leo ni maandamano ya watu. Watu wamejitokeza mtaani kusema hakuna ghasia zaidi, hakuna rushwa, hakuna uvivu zaidi, hakuna uzembe zaidi, hakuna utawala mbaya. Na kuunga mkono Brazil mpya." Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC

YANGA YAIADHIBU PLATNUM YA ZIMBABWE 5-1

Kikosi cha Yanga kilichoisambaratisha Platnum ya Zimbabwe kwa mabao 5-1
Timu pekee iliyobakia kwenye mashindano ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika kutoka Tanzania, Yanga, imeendelea kuweka matumaini hai ya kusonga mbele baada ya kuiangushia kipigo kikali timu ya Platnum ya Zimbabwe kwa mabao 5-1.
Mchezo huo wa raundi ya kwanza ya vilabu vinavyoshiriki Kombe la Shirikisho la CAF, ulifanyika Jumapili jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa kufungana mabao 2-1.
Kipindi cha Pili ndicho kilichokuwa kiama chya Platnum baada ya kuruhusu mabao matatu zaidi.
Wafungaji wa timu ya Yanga ni Mrisho Ngasa aliyefunga magoli mawili, Haruna Niyonzima, Salum Telela, na Amisi Tambwe walifunga bao moja kila mmoja. Kwa matokeo hayo Yanga imejenga mazingira ya kusonga mbele. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Sunday, March 15, 2015

ZITTO: IPO SIKU NITASHIKA NAFASI KUBWA TANZANIA

Wananchi wa Kijiji cha Nyalubanda wakiwa wamembeba Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alipowasili katika kijiji hicho jana katika hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa alilotoa ahadi katika kampeni za Uchaguzi wa mwaka 2010.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema kutimuliwa uanachama na Chadema ni dhoruba inayomkumba mwanasiasa yeyote anayefanikiwa na kwamba iko siku atashika “nafasi kubwa ya uongozi ya kuwatumikia Watanzania”.
Zitto aliwasili mjini hapa juzi, ikiwa ni siku chache baada ya Chadema kutangaza kumtimua uanachama kwa kosa la kupeleka mgogoro wa ndani ya chama kwenye mahakama.
Alifungua kesi Mahakama Kuu akitaka imuamuru katibu mkuu wa Chadema kumpa nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua madaraka yote na baadaye kukizuia chama hicho kumjadili. Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali shauri lake na Chadema ikatangaza mara moja kumtimua. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

PENGO ATOFAUTIANA NA MAASKOFU....!!!

 
Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akibariki matoleo yakiotolewa na Umoja wa Wanawake wa katoriki(WAWATA), wakati wa Ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam jana.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema waumini hawana budi kusoma vizuri na kuelewa Katiba Inayopendekezwa ili wakati ukifika, wafanbye uamuzi kwa hiari na utashi wao wakati wa kupiga Kura ya Maoni.
Ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku mbili baada ya Jukwaa la Wakristo kutoa tamko linalowataka waumini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura, kushiriki kikamilifu kwenye shughuli zote za elimu ya Katiba Inayopendekezwa na kupiga kura ya “hapana” kuikataa Katiba Inayopendekezwa.
Lakini jana, Kardinali Pengo alisema kuisoma na kuielewa katiba hiyo ndiyo wajibu wa msingi ambao Wakristo wanao kwa sasa ili kupiga kura inayostahili wakati ukifika. Kuhusu maaskofu kuagiza waumini waikatae Katiba Inayopendekezwa, Kardinali Pengo alisema wao wakiwa viongozi wa watu, hawana mamlaka wala uwezo huo, bali wenye uwezo ni wananchi wenyewe. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

LIPUMBA AKUBALI TAMKO LA MAASKOFU

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba  

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba ameunga mkono tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania kupinga Katiba Inayopendekezwa, akisema hoja zao ni za msingi kwa kuwa kuna mambo mengi yanayopingwa na wananchi.
Kauli ya Profesa Lipumba ni mwendelezo wa kauli tofauti zilizotolewa na watu mbalimbali kuhusu tamko la jukwaa hilo, wakiwamo wasomi, viongozi wa dini, wanaharakati na wanasiasa kuhusu hatima ya Kura ya Maoni na muswada wa Makahama ya Kadhi.
Alhamisi iliyopita, jukwaa hilo linaloundwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) liliwataka waumini wake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, kushiriki kikamilifu katika elimu ya Kura ya Maoni, na kisha kuipigia kura ya “hapana” Katiba Inayopendekezwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO MARCHI 15, 2015

.

.

.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MILIPUKO YALENGA MAKANISA...!!!

Wasichana walia kufuatia mashambulizi mawili yaliolenga makanisa Pakistan
Mabomu mawili yamelipuka yakilenga makanisa mawili yaliyokuwa yamejaa watu kwenye mji wa Lahore chini Pakistan wakati watu walipokuwa wakihudhuria misa ya jumapili.
Polisi wanasema kuwa takriban watu 6 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Mashambulizi hayo yanaoyoaminika kuwa ya kujitoa mhanga yalifanyika eneo lenye waumini wengi wa kikristo la Youhanabad
Sehemu ya kundi la Taliban linalofahamika kama Jamatul Ahra limesema kuwa ndilo lililoendesha shambulizi hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMO KUHUSU UBAKAJI KUFUNZWA UINGEREZA




Wanafunzi nchini Uingereza
Wanafunzi kuanzia miaka 11 nchini Uingereza watafundishwa kuhusu tofauti kati ya ubakaji na tendo la ngono ambalo limetekelezwa kutokana na idhini ya wapenzi wawili kama mojawapo ya mipango ya kuwawapa ujuzi kuhusu maisha ya sasa nchini humo
Somo hilo ambalo litaanzishwa mara moja baada ya siku kuu ya Easter litaongezwa katika mtaala wa Uingereza baada ya wasiwasi kutolewa kwamba vijana walikuwa wakishinikizwa kushiriki katika ngono.
Nick Morgan ambaye ni katibu wa elimu alitoa tangazo hilo siku ya kimataifa ya wanawake.
''Lazima swala hili tulikabili kwamba mambo ambayo wasichana wetu wanapitia hayakuwepo wakati wa ujana weyu,kwa hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa wasichana wetu wanamaliza shule wakiwa na uwezo wa kukabiliana na changaomoto watakazokumbana nazo wakiwa watu wazima'', aliandika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

VATICAN: NGUVU ZITUMIWE DHIDI YA IS

Askofu mkuu wa Vatican Silvano Tomasi
Makao makuu ya kanisa katoliki duniani Vatican yanasema kuwa nguvu inaweza kutumiwa kusitisha mashambulizi yanayoendeshwa na wanamgambo wa Islamic State dhidi ya wakristo na makundi mengine madogo .
Askofu mkuu Silvano Tomasi ambaye ni mwakilishi mkuu wa Vatican kwenye umoja wa mataifa mjini Geneva ameyashutumu makundi ya jihad kwa kuendesha mauaji ya halaiki.
Akizungumza kupitia mtandao wa Vatican amesema kuwa hatua za kijeshi zitaanzishwa ikiwa suluhu ya kisiasa haitapatikana.
Lakini amesema kuwa muungano wowote dhidi ya Islamic State ni lazima ujumuishe nchi za kiislamu kutoka mashariki ya kati. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAN UNITED KUMKOSA DI MARIA

Manchester United kumkosa nyota wake Angel Di Maria
Kilabu ya Manchester United itamkosa Angel Di Maria,ambaye anahudumia mafuruku ya mechi moja baada ya kupewa kadi nyekundi dhidi ya Arsenal,naye Jonny Evans akiwa anahudumia marufuku.
Mshambuliaji nyota Robbin Van Persie bado anauguza jeraha huku Marcos Rojo akiwa hajulikani iwapo atachezeshwa kutokana na jeraha la paja.
Hatahivyo Ashley Young atacheza licha ya kujiumiza mguu siku ya jumatatu.
Kocha wa kilabu ya Tottenham Mauricio Pochettino ana kikosi chake kizima.
Danny Rose huenda akacheza mechi ya leo katika safu ya ulinzi wa kushoto huku Mousa Dembele pia akitarajiwa kuanza. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WENGER: ARSENAL ITAIBANDUA MONACO

 kocha wa arsenal Arsene Wenger
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa kilabu hiyo bado ina fursa ya kuibandua Monaco katika michuano ya kilabu bingwa barani Ulaya licha ya kucharazwa 3-1 katika awamu ya kwanza ya mechi hizo.
Arsenal itakabiliana na timu hiyo ya Ligi ya daraja la kwanza siku ya jumapili huku ikiwa hakuna timu ilioweza kufanikiwa kubadilisha matokeo kama hayo katika michuano hiyo.
Wenger:Tuna changamoto kubwa mbele yetu lakini tutafanya kila kitu kuhakikisha kwamba tunafuzu kwa robo fainali.
''Wao ndio wanaopigiwa upato kufuzu lakini tunaweza kubadilisha mambo''.
''Tutahakikisha kuwa tuna hamu na imani ya kushinda''.
Kilabu ya Monaco inayotarajiwa kupepetana na Arsenal siku ya jumanne
Arsenal italazimika kufunga bao tatu kwa bila ili kuweza kufuzu kwa robo fainali.
Tayari kilabu hiyo imepata motisha kufuatia ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya kilabu ya West Ham siku ya jumamosi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Saturday, March 14, 2015

KINANA AMSIFU, AMPONDA NYARANDU...!!!



“Mfano ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye anafanya kazi ya kuzunguka nchi nzima na maeneo mengine wakati mizunguko yake haisaidii kuondoa matatizo ya wananchi.” Kinana 

Jana ilikuwa siku ya hisia tofauti kwa watu wawili wanaotajwa kwenye kinyang’anyiro cha urais, Edward Lowassa na Lazaro Nyalandu baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kumsifu mmojawao na kumponda mwingine.
Akiwa Kondoa, Kinana alitumia muda mwingi kujibu kilio cha wananchi wanaosumbuliwa na askari wa wanyamapori kwa kumponda Waziri Nyalandu kuwa anazurura bila kushughulikia matatizo ya wananchi, lakini saa chache baada ya kuwasili Monduli alimsifu Lowassa kuwa ni kiongozi shupavu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO MARCHI 14, 2015

.
.
.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

UNENE WAMKOSESHA BURUDANI


klabu ya burudani nchini Uingereza
Mama mmoja amedai kuwa yeye na marafiki zake wawili walizuiliwa kuingia katika kilabu moja ya burudani kwa sababu zinazodaiwa kuwa ni wanene sana na wenye sura mbaya
Stacey Owen 33, alikuwa ametoka na marafiki zake wawili kwa ajili ya kupata burudani wakati wa usiku siku ya jumamosi alipokataliwa kuingia katika baa moja jijini Manchester kwa sababu ya unene wake.
Stacey amesema wao walizuiwa huku watu wengine wakiingia katika baa hiyo maarufu mjini humo,
Klabu ya burudani Uingereza
Mama huyo sasa anataka kuombwa radhi na wamiliki wa Baa hiyo lakini mpaka sasa amedai hajapata ujumbe wowote kutoka kwao.
Anasema sio kwamba anajiona kwamba yeye ni mrembo sana lakini kilichomshangaza ni uwepo wa ubaguzi huo miongoni mwa wateja. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Friday, March 13, 2015

HUYU NDIYE MTOTO ALIYENUSURIKA KIFO KWENYE AJALI YA BASI YA MAJINJA PALE CHANGARAWE MUFINDI


Hapa mtoto huyo akiendelea kutibiwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi. Tupia neno moja kwa mtoto huyu ili kumtakia afya njema katika
Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SERIKALI KUJENGA NYUMBA 403 MWAKATA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuwafariji waathirika wa Mvua ya Mawe,iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata,Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga.

Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali itajenga nyumba 403 ambazo zimebomolewa na mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu 649 kukosa mahali pa kuishi.
Kauli hiyo aliitoa jana kwenye kijiji cha Mwakata baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa na mvua hiyo na kujionea maisha duni wanayoishi watu hao.
Akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wake Rais Kikwete alisema Serikali iko pamoja na wananchi hao na itahakikisha makazi yao yanarejea katika hali yake ya kawaida kwa kuwajengea nyumba hizo.
Pia, Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) wajenge nyumba hizo bila kupitia mkandarasi yeyote kama vile ulivyo ujenzi wa Serikali kwa kuwa ujenzi wa jeshi unaisha kwa muda mfupi na hakuna uchakachuaji. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MKUU WA WILAYA YA MUFINDI MH. MBONI MHITA AUNDA KAMATI MAALUMU YA KUCHUNGUZA CHANZO CHA AJALI YA CHANGARAWE

 Mh. Mboni Mhita akizungumza na moja wa majeruhi katika hospitali ya wilaya ya Mufindi

 Mkuu wa wilaya akiwa na wana kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo eneo la tukio

Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAASKOFU: PIGIENI KATIBA KURA YA HAPANA


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa      


Jukwaa la Wakristo Tanzania limewataka waumini wake kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa kwa kupiga kura ya “hapana”.

Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo jana na kusainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet, imetaja sababu mbili za uamuzi wake kuwa ni muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini, na Kura ya Maoni kusababisha mgawanyiko.

“Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa hapo juu,” linasema tamko hilo la kurasa nne.Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO MARCHI 13, 2015

.
 
.

.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WATOTO WENGINE 11 WAKUTWA WAMEFICHWA

 
 Baadhi ya watoto 18 katika tukio la kwanza walikuwa wakihifadhiwa kwenye nyumba iliyopo Kata ya Pasua kwa lengo la kuwafundisha dini ya Kiislamu, mkoani Kilimanjaro.

Mambo mazito zaidi yamezidi kubainika mkoani Kilimanjaro baada ya polisi kugundua nyumba nyingine yenye watoto kumi na mmoja waliokusanywa kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya kufundishwa dini.
Hii ni mara ya pili katika muda usiozidi wiki moja baada ya polisi kubaini nyumba iliyohifadhi watoto 18 kwa lengo kama hilo Jumamosi iliyopita.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela alisema tukio hilo linafanya wapelelezi kuumiza vichwa kwa kuwa mikoa waliyotoka ndio ile ile waliyotoka watoto 18 waliokutwa kwenye nyumba moja mjini Moshi.
Nyumba hiyo imebainika wakati kukiwa na madai kwamba baadhi ya misikiti katika maeneo ya Pasua, Njoro na Kibosho yanaendesha mafunzo ya judo na karate. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KESI YA KENYATTA YAFUNGWA RASMI

Kesi ya rais wa kenya Uhuru kenyatta imefungwa rasmi
Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta .
Alikuwa ameshtakiwa na uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Mwezi Disemba kiongozi wa mashtaka alimuondolea mashtaka kiongozi huyo akisema kuwa serikali ya Kenya imekataa kuipatia mahakama hiyo ushahidi muhimu.
Hatahivyo mahakama hiyo imesema kuwa upande wa mashtaka una uwezo wa kuanzisha mashtaka mapya katika siku za usoni iwapo ina ushahidi wa kutosha.
Kesi ya naibu wa rais William Ruto inaendelea katika mahakama hiyo.
Mawakili wake walishindwa kuiondoa kesi yake. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

GAVANA ANUSURIKA KIFO KENYA

 Gavana Ali Roba wa kaunti ya Mandera
Mwanasiasa mmoja wa Kenya amenusurika shambulizi lililotekelezwa na kundi la Al shabaab.
Ali Roba ,ambaye ni gavana wa mji ulio mpakani wa Mandera alikuwa akisafiri kuelekea mjini humo wakati msafara wake ulipovamiwa.
Jaribio hilo sio la kwanza kuhusu maisha ya mwanasiasa huyo ambaye amekuwa akiongoza kampeni dhidi ya kundi hilo katika eneo hilo.
Wapiganaji hao tayari wamekiri kutekeleza shambulizi hilo na kusema wamefanikiwa kuwaua wanajeshi wanne,kuchoma magari mawili na kutoroka na jengine.
Kufikia sasa polisi wa Kenya hawajathibitisha matamshi hayo ya kundi hilo.
Al shabaab
Tukio hilo lilitokea katika barabara ambapo watu 28 waliokuwa wakisafiri katika basi walivamiwa na kuuawa miezi minne iliopita.
Barabara hiyo iko karibu na mpaka na Somali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ALGERIA TIMU BORA AFRIKA

Algeria imesalia katika nafasi ya kwanza katika orodha mpya ya timu bora barani Afrika
Algeria imesalia timu bora barani Afrika katika orodha ya FIFA ya mwezi March licha ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha kombe la mataifa bingwa ya Afrika na Ivory Coast.
''The Desert Foxes'' walitupwa nje ya mashindano hayo na The Elephants ya Ivory Coast katika hatua ya robo fainali.
Hata hivyo ushindi huo wa ''The Elephants'' huko Equatorial Guinea, mabingwa hao waliwapiku kwenye orodha hiyo mpya iliyotolewa Alhamisi.
Algeria wameorodheshwa katika nafasi ya 18 duniani huku Ivory Coast ikiorodheshwa ya 20 duniani .
Black stars ya Ghana ni timu ya tatu kwa ubora barani lakini imeorodheshwa katika nafasi ya 24 duniani.
Tunisia ni ya nne barani Afrika lakini ya 25 duniani.
Senegal inafunga orodha ya tano bora barani Afrika.
Mabingwa wa kombe la mataifa ya Afrika Ivory Coast
Timu hiyo hata hivyo imeorodheshwa katika nafasi ya 36 duniani. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kwa mara ya Kwanza wenyeji wa kombe la mataifa bingwa ya Afrika Equatorial Guinea wameondolewa katika nafasi kumi bora barani afrika licha ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye kipute hicho cha mwaka huu.
Orodha ya nafasi kumi bora barani Afrika.
1 (18). Algeria
2 (20). Ivory Coast
3 (24). Ghana
4 (25). Tunisia
5 (36). Senegal
6 (38). Cape Verde
7 (41). Nigeria
8 (44). Guinea
9 (47). DR Congo
10 (49). Cameroo

CHAMBERLAIN KUKAA NJE MWEZI MMOJA

 Alex Oxlade-Chamberlain hatokuwepo kwa mwezi mmoja
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atalazimika kujikuna kichwa baada ya kupata habari kuwa kiungo chake cha kutegemewa Alex Oxlade-
Chamberlainhatakuwepo kwa takriban majuma tatu hadi nne zijazo kutokana na jeraha nyuma ya goti.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kulingana na kocha huyo,Chamberlain alipata jeraha hilo katika mechi ya kukata na shoka ya FA dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester United jumatatu iliyopita.
Kujeruhiwa kwake ni pigo kwa azimio la Arsenal kuimarisha matokeo yao katika ligi kuu ya Uingereza ambapo sasa wanashikilia nafasi ya tatu .
Alex Oxlade-Chamberlain alichangia pakubwa katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester united katika FA
Aidha Arsenal wanajiandaa kwa mechi ya marudio ya mkondo wa 16 bora katika ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya ambapo wameratibiwa kuchuana dhidi ya Monaco juma lijalo.
Winga huyo alikuwa amerejea mwishoni mwa mwezi Februari baada ya kukaa mwezi mmoja nje kufuata jeraha lengine la kiuno.
Wenger hata hivyo alipata afueni katika safu ya ulinzi baada ya kurejea kwa Gabriel aliyejeruhiwa katika mechi ngumu dhidi ya QPR mnamo Machi tarehe 4.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

FORLAN ATUNDIKA DARUGA KIMATAIFA

IMG_20150312_202943
Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Manchester United, Atletico Madrid, Intermilan Diego Forlan jana ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Uruguay baada ya kuichezea timu hiyo tangu mwaka 2002.
Forlan,35, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Cerezo Osaka ya nchini Japan amekuwa msaada mkubwa kwa timu ya taifa ya Uruguay na mwaka 2010 aliiwezesha timu hiyo kushinda nafasi ya 3 kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika huko nchini Afrika kusini huku yeye akibeba tuzo ya mchezaji bora wa mashindano hayo baada kuonesha kiwango bora.
“Ninawashukuru kwa wote walionipa ushirikiano tangu naanza kuichezea timu ya taifa mwaka 2002, ninaamini timu itaendelea kufanya vizuri na nimechukua uamuzi huu ili kutoa kwa nafasi kwa wachezaji wengine ambao ninatumaini wataisadia timu hii” alisema Forlan.
Mchezaji huyo aliyepata sifa nyingi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira ya adhabu mpaka anatangaza kustaafu tayari ameshaichezea timu ya taifa ya Uruguay michezo 112 na kufunga magoli 36. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Thursday, March 12, 2015

KONTENA LALALIA BASI, LAUA WATU 42, LAJERUHI 23

Basi la Majinja likiwa limeangukiwa na kontena na kusababisha vifo katika eneo la Changalawe mafinga.

Watu 42 wamepoteza maisha na wengine 23 kujeruhiwa baada ya lori la mizigo kugongana na basi na kontena lililokuwa limebebwa kuangukia gari hilo la abiria, katika ajali ya aina yake iliyotokea eneo la Mafinga Changalawe mkoani Iringa.
Watu 37 waliokuwa kwenye basi hilo la kampuni ya Majinjah Express lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam, walifariki papo hapo na wengine watano kufariki wakiwa Hospitali ya Mafinga. Dereva wa basi na wa lori hilo la kampuni ya Cipex, pia wamefariki.
Shuhuda mmoja wa ajali hiyo, Nyasio Pascal, aliyekuwa akiendesha basi la Saibaba, alisema aliliona lori hilo likijaribu kukwepa mashimo kwenye barabara hiyo ambayo ni nyembamba, na mara likaanza kuyumba kulia na kushoto baada ya kukanyaga shimo na ndipo lilipolifuata basi na kugongana nalo.
Alisema kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo, liliangukia juu ya basi na kulikandamiza, jambo ambalo lilisababisha vifo vya watu wengi na pia kuzuia watu waliokuwa karibu na ajali kuokoa watu waliojeruhiwa hadi tingatinga lilipowasili. Hata hivyo, alisema mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja, alinusurika kwenye ajali hiyo bila ya kudhurika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

NENO KUTOKA YEREMIA 32:27 LILILOPO KWENYE KAMPUNI YA MAJINJA SPECIAL

Yeremia 32 : 27
"Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?"

ZITTO KABWE KUIBUKIA KIGOMA KESHO

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe  

Siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kumvua uanachama, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kesho atatua jimboni kwake kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Uamuzi wa kumfukuza Zitto (pichani) ulifikiwa juzi ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi aliyofungua Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya Wadhamini na katibu mkuu wa Chadema, iliyokuwa imeshikilia uanachama wake.
Mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ndiye alitangaza kutimuliwa kwa Zitto akisema ni kutokana na kufungua kesi mahakamani, kinyume na Katiba ya Chadema kipengele cha 8 (a) (x). Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO MARCHI 12, 2015


..
. 


. 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

CHEYO AKARIBISHA 'WAGENI' KUWANIA URAIS UDP

Mwenyekiti wa UDp, John Cheyo. 

Mbunge wa Bariadi  Mashariki na Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo  amesema wanakaribisha wanachama wa chama chochote cha siasa nchini kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam, kiongozi huyo alisema chama hicho bado hakijateua mgombea  urais hivyo milango iko wazi kwa wanasiasa ambao wako tayari kujiunga na chama hicho kwa lengo la kuwania urais.
“Hiki chama ni cha watanzania wote hivyo tunatoa rai kwa mtu yeyote  aliye tayari kuwa mwanachama wetu milango ya kuwania urais kupitia chama hiki ipo wazi’’ alisema Cheyo
Alisema  yeye bado hajaamua kuwania nafasi hiyo kwa sasa muda ukifika atasema lakini kwa sasa ni mapema kutoa tamko kwamba atawania wadhifa huo.
Aliongeza kwamba  anasikitishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwahamasisha watu wasipigie kura Katiba inayopendekezwa, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwanyima haki wananchi.
‘’Raia wote wana haki ya kupiga kura sasa ikiwa Ukawa wanatembea kila kona ya nchi kuwahamasisha wananchi kuacha kuipigia kura katiba hiyo ni kosa,’’ alisema Cheyo
Pia Kiongozi huyo wa UDP alisema tume ya uchaguzi ndio yenye majibu ya mashine zinazotumika kuandikisha wapiga kura  kwenye daftari la kudumu, (BVR) kwamba zinafaa au hazifai.
Alisema anashangazwa sana na baadhi ya watu hususan wanasiasa na wasomi wanaojitokeza na kusema mchakato wa kuandikisha wapiga kura usimamishwe kwa sababu zao mbalimbali . Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

IS WANATUMIA GESI YA KLORINI IRAQ



Wapiganaji nchini Iraq
Shirika la Utangazaji -BBC- limepata ushahidi unaoonyesha wapiganaji wa wa Islamic State wanatumia gesi ya Klorini.
Gesi hiyo huwekwa kwenye silaha za kemikali katika vita nchini Iraq.
Serikali ya Iraq imesema kiasi kidogo cha kemikali kimekuwa kikitumika katika mabomu yanayolenga majeshi yake ambayo yamekuwa yakiwaondoa wapiganaji Islamic State katika mji wa Tikrit.
Katika picha video ambayo BBC imeoneshwa na kikosi cha kuharibu mabomu nchini Iraq imeonekana mlipuko wa bomu ukiwa na moshi wa rangi ya chungwa ukipaa angani.
Bomu hilo lilikuwa na kiasi kidogo cha Klorini ambayo huenda hutumika kama sumu kwenye maeneo ya wazi.
Kumekuwa na taarifa za wapigani wa Islamic State kutumia gesi ya klorini tangu walipoanza harakati zao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...