Sunday, March 15, 2015

ZITTO: IPO SIKU NITASHIKA NAFASI KUBWA TANZANIA

Wananchi wa Kijiji cha Nyalubanda wakiwa wamembeba Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alipowasili katika kijiji hicho jana katika hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa alilotoa ahadi katika kampeni za Uchaguzi wa mwaka 2010.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema kutimuliwa uanachama na Chadema ni dhoruba inayomkumba mwanasiasa yeyote anayefanikiwa na kwamba iko siku atashika “nafasi kubwa ya uongozi ya kuwatumikia Watanzania”.
Zitto aliwasili mjini hapa juzi, ikiwa ni siku chache baada ya Chadema kutangaza kumtimua uanachama kwa kosa la kupeleka mgogoro wa ndani ya chama kwenye mahakama.
Alifungua kesi Mahakama Kuu akitaka imuamuru katibu mkuu wa Chadema kumpa nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua madaraka yote na baadaye kukizuia chama hicho kumjadili. Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali shauri lake na Chadema ikatangaza mara moja kumtimua. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Akihutubia mamia ya watu kwenye Kijiji cha Nyarubanda ambako alikabidhi gari la wagonjwa, Zitto aliwatoa hofu wananchi hao walioonyesha shauku ya kujua hatma yake na kuwaeleza kuwa hajawatupa, ataendelea kuwahudumia.
“Hakuna kiongozi aliyefanikiwa kisiasa bila kupitia misukosuko ya kupingwa,” alisema Zitto ambaye anamalizia kipindi cha pili cha ubunge wake kwenye jimbo hilo.
“Waziri Mkuu za zamani ya India, Indira Gandhi alifukuzwa na chama chake na aliamua kuunda chama kipya na baadaye kuwashinda waliomfukuza katika uchaguzi. Kwa hiyo nawatoa hofu kwa maana ninajengwa zaidi kisiasa.
“Nipo kwenye dhoruba ambayo inanijenga kisiasa na ipo siku nitawatumikia Watanzania katika nyadhifa kubwa za uongozi.” Katika mkutano huo ambao wananchi walimpokea wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kama “Mheshimiwa Zitto tulikuchagua wewe na siyo chama,” huku mengine yakiandikwa “chama siyo bora, ubora ni utendaji kazi”.
Viongozi mbalimbali wa CCM na vyama vingine vya siasa walijumuika kwenye uwanja huo kumpokea Zitto na kushiriki naye kucheza ngoma za asili.
Baadhi ya viongozi hao ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Hamisi Betese, mkurugenzi wa halmashari hiyo, Michael Mwandezi na viongozi wengine wa serikali za mitaa.
Akiongea katika hadhara hiyo, Betese alisema kuwa kitendo cha Zitto kutoa gari ambayo aliwaahidi wananchi kipindi cha uchaguzi ni utekelezaji wa ilani ya CCM ambayo ndiyo chama tawala.
Aliongeza kuwa yeye kama mwenyekiti wa halmashauri bado anamtambua Zitto kama mbunge wa Kigoma Kaskazini mpaka hapo taarifa rasmi zitakapotolewa.
Wanakijiji hao walishukuru Zitto kwa kutoa gari hilo wakisema litawasaidia kuokoa fedha nyingi walizokuwa wakitumia kutafuta magari binafsi wanapokuwa na wagonjwa wanaohitaji matibabu ya haraka. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...