Mwanasiasa mmoja wa Kenya amenusurika shambulizi lililotekelezwa na kundi la Al shabaab.
Ali Roba ,ambaye ni gavana wa mji ulio mpakani wa Mandera alikuwa akisafiri kuelekea mjini humo wakati msafara wake ulipovamiwa.
Jaribio
hilo sio la kwanza kuhusu maisha ya mwanasiasa huyo ambaye amekuwa
akiongoza kampeni dhidi ya kundi hilo katika eneo hilo.
Wapiganaji
hao tayari wamekiri kutekeleza shambulizi hilo na kusema wamefanikiwa
kuwaua wanajeshi wanne,kuchoma magari mawili na kutoroka na jengine.
Kufikia sasa polisi wa Kenya hawajathibitisha matamshi hayo ya kundi hilo.
Tukio hilo lilitokea katika barabara ambapo watu 28 waliokuwa wakisafiri katika basi walivamiwa na kuuawa miezi minne iliopita.
Barabara hiyo iko karibu na mpaka na Somali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment