Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta .
Alikuwa ameshtakiwa na uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Mwezi
Disemba kiongozi wa mashtaka alimuondolea mashtaka kiongozi huyo
akisema kuwa serikali ya Kenya imekataa kuipatia mahakama hiyo ushahidi
muhimu.
Hatahivyo mahakama hiyo imesema kuwa upande wa mashtaka
una uwezo wa kuanzisha mashtaka mapya katika siku za usoni iwapo ina
ushahidi wa kutosha.
Kesi ya naibu wa rais William Ruto inaendelea katika mahakama hiyo.
Mawakili
wake walishindwa kuiondoa kesi yake. Tangaza biashara yako hapa kwa bei
nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/
Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment