Algeria
imesalia timu bora barani Afrika katika orodha ya FIFA ya mwezi March
licha ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha kombe la mataifa bingwa ya
Afrika na Ivory Coast.
''The Desert Foxes'' walitupwa nje ya mashindano hayo na The Elephants ya Ivory Coast katika hatua ya robo fainali.
Hata
hivyo ushindi huo wa ''The Elephants'' huko Equatorial Guinea, mabingwa
hao waliwapiku kwenye orodha hiyo mpya iliyotolewa Alhamisi.
Algeria wameorodheshwa katika nafasi ya 18 duniani huku Ivory Coast ikiorodheshwa ya 20 duniani .
Black stars ya Ghana ni timu ya tatu kwa ubora barani lakini imeorodheshwa katika nafasi ya 24 duniani.
Tunisia ni ya nne barani Afrika lakini ya 25 duniani.
Senegal inafunga orodha ya tano bora barani Afrika.
Timu hiyo hata hivyo imeorodheshwa katika nafasi ya 36 duniani. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kwa
mara ya Kwanza wenyeji wa kombe la mataifa bingwa ya Afrika Equatorial
Guinea wameondolewa katika nafasi kumi bora barani afrika licha ya
kumaliza katika nafasi ya nne kwenye kipute hicho cha mwaka huu.
Orodha ya nafasi kumi bora barani Afrika.
1 (18). Algeria
2 (20). Ivory Coast
3 (24). Ghana
4 (25). Tunisia
5 (36). Senegal
6 (38). Cape Verde
7 (41). Nigeria
8 (44). Guinea
9 (47). DR Congo
10 (49). Cameroo
No comments:
Post a Comment