Shirika la Utangazaji -BBC- limepata ushahidi unaoonyesha wapiganaji wa wa Islamic State wanatumia gesi ya Klorini.
Gesi hiyo huwekwa kwenye silaha za kemikali katika vita nchini Iraq.
Serikali
ya Iraq imesema kiasi kidogo cha kemikali kimekuwa kikitumika katika
mabomu yanayolenga majeshi yake ambayo yamekuwa yakiwaondoa wapiganaji
Islamic State katika mji wa Tikrit.
Katika picha video ambayo BBC
imeoneshwa na kikosi cha kuharibu mabomu nchini Iraq imeonekana mlipuko
wa bomu ukiwa na moshi wa rangi ya chungwa ukipaa angani.
Bomu hilo lilikuwa na kiasi kidogo cha Klorini ambayo huenda hutumika kama sumu kwenye maeneo ya wazi.
Kumekuwa na taarifa za wapigani wa Islamic State kutumia gesi ya klorini tangu walipoanza harakati zao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment