Ripoti
ya mashirika zaidi ya ishirini ya misaada ya kibinadamu na yale ya
kutetea haki za binaadamu yamelishutumu Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa kwa kushindwa kutetea raia walio katikati ya vita nchini Syria.
Ripoti
hiyo imezishutumu nchi zenye nguvu kubwa ya ushawishi duniani kwa
kushindwa kutumia nguvu zao kuandaa maazimio ya kusaidia uhuru wa huduma
za misaada ya kibinadamu kwa waathirika.
Ripoti ya masharika hayo ni ya kuadhimisha miaka minne ya vita nchini Syria ambavyo vinaendelea hadi hivi sasa.
David
Milband ambaye ni Rais wa Shirika la kimataifa la Uokoaji International
Rescue Committee amesema kuna ongezeko dogo la misaada inayotolewa
kuwasaidia raia wa Syria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment