Monday, June 20, 2016

YANGA YASHINDWA KUTAMBA KWA WAARABU YAPIGWA 1-0

 Mabingwa wa soka la Tanzania bara Yanga SC wameanza vibaya kampeni zao za kuwania kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya MO Bejaia ukiwa ni chezo wa Kundi A.

Yassin Sahli alifunga bao pekee kwenye mchezo huo na kuipa pointi tatu MO Bejaia iliyokuwa ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani Stade de I’Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria.
Matokeo hayo yanaiacha Yanga katika nafasi ya tatu huku TP Mazembe wakiwa ndiyo vinara wa Kundi baada ya kushinda mchezo wao kwa magoli 3-0 dhidi ya Medeama ambayo inaburuza mkia.

Mazembe na MO Bejaia zinapointi sawa (pointi tatu) lakini TP Mazembe anaongoza kundi kwa tofauti ya magoli wakati Yanga na Medeama zikiwa hazina pointi lakini Yanga inakaa nafasi ya tatu kwa tofauti ya magoli. Medeama imefungwa magoli matatu wakati Yanga wameruhusu bao moja pekee.
Mchezo ujao wa Yanga utakuwa nyumbani (Dar es Salaam) June 28 itakapowaalika TP Mazembe kwenye uwanja wa taifa.

1 comment:

Winnie said...

Waooh I love this. Can I download

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...