Timu
ya Bayern Munich ya Ujerumani na Paris St. Germain ya Ufaransa
zimesonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa
barani Ulaya kufuatia matokeo waliyayapata usiku wa kuamkia leo.
Wakicheza
kwa kujiamini Bayern Munich ilidhihirisha kuwa ni moto wa kuotea mbali
katika mashandano hayo baada ya baada ya kuwapa kichapo cha mbwa mwizi
wapinzani wao Shakhtar Donetsk ya Ukrine cha magoli 7- kwa mtungi.
Magoli
ya Bayern Munich yalitiwa kimiani na Thomas Muller, Jerome Boateng
,Franck Ribery,Holger Bastuber, Robert Lewandowski na Mario Gotze.
Nayo
Paris St. Germain ya Ufaransa imesonga mbele hatua ya robo fainali
baada ya kuwaondoa Chelsea katika mashindano hayo japo timu hizo
zilitoka sare ya magoli mawili kwa miwili lakini magoli ya ugenini
iliyoyafunga hapo jana ndio yaliyowanufaisha Paris St. Germain.
Hivyo
mshindi katika mechi hiyo ilibidi kupatikana katika dakika thelathini
za nyongeza baada ya dakika tisini za kawaida kumalizika huku timu zote
zikiwa zimefungana goli moja kwa moja.
Wakiwa na matumaini ya
kuingia robo fainali Chelsea ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli
kupitia Gary Cahill katika 81 lakini Mlinzi wa zamani wa Chelsea David
Luiz akafutilia ndoto hizo mbali baada ya kusawazisha goli hilo katika
dakika ya 86.
Na hivyo hadi dakika 90 za kwanza zinamalizika
Chelsea 1 na Paris St. Germain 1 na hivyo kulazimika kucheza dakika 30
nyingine ili kumpata mshindi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment