Zaidi
ya watu milioni moja kutoka nchini Brazil wameandamana dhidi ya rais wa
nchi hiyo Dilma Rousseff, huku wengi wao wakitaka rais huyo afunguliwe
mashtaka ya ufisadi mkubwa uliofanyika katika shirika la mafuta la
serikali, Petrobras.
Maandamano kama hayo yamefanyika katika miji mingi ya Brazil ikiwemo mji mkuu wa nchi hiyo Brasilia.
Maandamano makubwa kabisa yamefanyika katika mji wa Sao Paulo ambalo ni eneo la upinzani waliokuwa wakipita mitaani.
Mmoja wa waandamanaji Francisco Pestana alilalama akisema"Dilma hana
uwezo wa kuongoza nchi yetu. Tunachokabiliwa nacho ni bahati mbaya sana,
namna mamabo yanavyokwenda, yanaweza kuelekea kubaya zaidi, tutakuwa
Venezuela nyingine."
Naye mwandamanaji mwingine mwanamke Janaina
Lima anasema "leo ni maandamano ya watu. Watu wamejitokeza mtaani kusema
hakuna ghasia zaidi, hakuna rushwa, hakuna uvivu zaidi, hakuna uzembe
zaidi, hakuna utawala mbaya. Na kuunga mkono Brazil mpya." Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC
No comments:
Post a Comment