Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe amesema chama hakitasita kumvua wadhifa yeyote atakayebainika
kuchaguliwa kwa kutoa rushwa.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana katika Mkutano Mkuu
wa Baraza la Vijana wa Chama hicho, (Bavicha) kabla ya kufanyika kwa
uchaguzi wa viongozi watakaoliongoza baraza hilo kwa miaka mitano.
“Hatutawavumilia watakaoshinda kwa rushwa,
kinachotakiwa ni wanachama kuchagua viongozi watakaokipeleka mbele
chama, chagueni vijana makini na watakaokipeleka chama kushinda chaguzi
za vitongoji, serikali za mitaa, udiwani, ubunge na hatimaye uchaguzi
mkuu,” alisema Mbowe.
Mbowe, ambaye ni Mbunge wa Hai na kiongozi wa
kambi rasmi ya upinzani bungeni aliwahadharisha viongozi watakaopatikana
kuhakikisha wanakwenda kuendeleza mapambano. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz