Amesema si kila mtu anayetaka serikali tatu
anaupenda Muungano na kusisitiza kuwa ni aibu kuwa na marais watatu
ndani ya nchi moja.
“Msimamo wangu wa serikali tatu si msimamo wa
marais watatu kwa sababu najua msimamo wa marais watatu utavunja nchi.
Msimamo wangu ni rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano, Mkuu wa Serikali
Zanzibar na Mkuu wa Serikali Bara,” alisema.
Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya
Chadema, moja ya vyama vinavyounda Ukawa, alitoa ufafanuzi huo wiki
iliyopita katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Masaki,
Dar es Salaam. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Pamoja na Chadema, Ukawa inaundwa na vyama vya CUF
na NCCR-Mageuzi pamoja na wajumbe wachache wa Kundi la 201 ambao
walisusia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba tangu Aprili 16, mwaka huu,
wakitaka ijadiliwe Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Marekebisho
ya Katiba yenye kupendekeza muungano wa serikali tatu badala ya mbili
zinazopendekezwa na CCM.
Akieleza sababu za kutoungana na Ukawa, Zitto
alisema baadhi ya wajumbe wake wanasema njia nyepesi ya kubakia na
Zanzibar ni serikali tatu, wengine wanasema njia nyepesi ya kubakia na
Tanganyika ni serikali tatu, “Binafsi ni muumini wa Muungano na dola
duniani kote hazivunjwi, bali zinaimarishwa.”
Kuhusu muungano anaoupendekeza alisema: “Chama
chenye wawakilishi wengi kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar kitatoa
Mkuu wa Serikali Zanzibar na chama chenye wabunge wengi Baraza la
Wawakilishi Tanganyika kitatoa Mkuu wa Serikali Tanganyika na Bunge liwe
moja.”
Alisema anachofikiria ni namna ya kuzifanya nchi
za Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya zinakuwa pamoja na Tanzania na si
kujadili namna ya kuzitenganisha na Tanzania.
“Tumeona Ethiopia na Eritrea zilivyotengana. Nini
kimetokea pale Wasudani walipoamua kujitenga wenyewe kwa wenyewe.
Tujifunze kwa mifano hii, hatuwezi kuwa na wakuu wa nchi watatu ndani ya
nchi moja, tutachekwa na dunia. “Lakini kwa sababu wenye sauti za
kuukataa muungano ni wengi zaidi katika Ukawa lakini hawawezi
kujionyesha, mimi siwezi kuwa nao na nipo wazi kabisa.”
Alisema Ukawa walimwalika katika vikao Dodoma
wakati Bunge la Katiba linaanza lakini aliwakatalia na kuwaeleza kuwa
miongoni mwao wapo wanaotaka muungano uvunjike.
Kuhusu kuingia bungeni alisema: “Siendi katika
vikao vya Bunge la Katiba kwa sababu ni kupoteza muda tu. Huwezi
kutengeneza Katiba ya nchi bila maridhiano. Lazima mridhiane ndipo mkae
mtengeneze. Katiba haina mshindi.”
Alisema kitendo cha baadhi ya wajumbe kususia
vikao na wengine kuendelea si jambo la kufurahia kwa kuwa Katiba inaweza
kupata uhalali wa kisheria lakini ikakosa uhalali wa kisiasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment