Mtoto wa
aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi
wakati wa mapambano na wanamgambo wa kiislamu Boko Haram.
Luteni
Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa siku ya jumatatu wakati jeshi la
Nigeria lilipokuwa likipambana kuudhibiti mji wa Michika karibu na mji
wa Mubi mji uliokuwa ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la Adamawa.Msemaji wa zamani wa Olusegun Obasanjo ameiambia BBC kuwa kanali Adeboye anaendela vizuri.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao, wanajeshi wameondoka kwenye kambi za kijeshi na chuo katika jimbo hilo kufungwa.
Wanamgambo wa Boko haram wamedhibiti miji mingi kaskazini mashariki na kutangaza kuwa himaya za kiislamu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
No comments:
Post a Comment