Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe amesema chama hakitasita kumvua wadhifa yeyote atakayebainika
kuchaguliwa kwa kutoa rushwa.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana katika Mkutano Mkuu
wa Baraza la Vijana wa Chama hicho, (Bavicha) kabla ya kufanyika kwa
uchaguzi wa viongozi watakaoliongoza baraza hilo kwa miaka mitano.
“Hatutawavumilia watakaoshinda kwa rushwa,
kinachotakiwa ni wanachama kuchagua viongozi watakaokipeleka mbele
chama, chagueni vijana makini na watakaokipeleka chama kushinda chaguzi
za vitongoji, serikali za mitaa, udiwani, ubunge na hatimaye uchaguzi
mkuu,” alisema Mbowe.
Mbowe, ambaye ni Mbunge wa Hai na kiongozi wa
kambi rasmi ya upinzani bungeni aliwahadharisha viongozi watakaopatikana
kuhakikisha wanakwenda kuendeleza mapambano. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Iwe ni marufuku kuruhusu nafasi yoyote eti
kiongozi wa CCM anapita bila kupingwa, wa CCM akipita hivyo na wewe
jiandae kuwajibika na sisi Ukawa hatutagombea nafasi tutaangalia jinsi
gani tutaweza kushirikiana hadi kuiondoa CCM madarakani mwakani,”
alisema Mbowe huku akishangiliwa na wajumbe wa mkutano huo.
Mbowe alivishauri vyama vya CUF na NCCR-Mageuzi
kuendeleza harakati za kujijenga kila chama kwa namna yake ili
utakapofika wakati wa kuunganisha nguvu iwe rahisi kushinda uchaguzi.
Naye Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Bavicha,
John Heche alisema chama hicho kwa sasa kimeimarika kuanzia ngazi ya
misingi hadi mikoa na kufikia matawi 350.
“Ninyi vijana chagueni viongozi makini,
watakaokitoa chama hapa kilipo kukipeleka mbele zaidi, wapo waliopoteza
uhai, kujeruhiwa na kupoteza mali zao kwa ajili ya Chadema hivyo
unapopata dhamana ya kuwa kiongozi ndani ya Chadema itumie vizuri,”
alisema Heche.
Uchaguzi wa viongozi kuongoza baraza hilo, ulikuwa ukiendelea wakati gazeti hili likienda mitamboni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment