Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa akizungumza na wenyeviti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia (kulia) na Ibrahim Lipumba baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wahabari kuhusu mchakato wa Katiba na Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), umemtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba (BMK), Samuel
Sitta kusitisha vikao vya Bunge sasa mpaka mwafaka utakapopatikana kwa
kuwa kuendelea kwake kunahalalisha ulaji wa fedha za walipakodi.
Akisoma tamko la vyama hivyo mbele ya wanahabari
jana, Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia, alisema: “Ukawa tunapaza
sauti zetu, tukisema hapana! Hapana! Haikubaliki.”
Alisema kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete na Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD), wameafikiana kuahirishwa kwa Bunge hilo
kupisha maandalizi ya Bunge la Muungano wa Tanzania, kuendelea kwa BMK
hadi Oktoba 4 ni ufujaji wa fedha za umma.
Mbatia alisema TCD walikubaliana kuwa mchakato wa Katiba hauwezi kufikia mwisho sasa kutokana na mambo kadhaa kutokwenda sawa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi, aliongeza kuwa
mchakato huo unapita katika kipindi kigumu na tete ambacho kama hatua
madhubuti hazitachukuliwa, Tanzania inaweza kuingia katika machafuko
yatakayochafua taswira yake duniani.
Alisema wajumbe wa TCD walikubaliana kufanya
mabadiliko ya 15 ya Katiba ya sasa na pia kutoa nafasi kwa mazungumzo
yanayoendelea ya kupata maridhiano ya kisiasa juu ya Katiba itakayowafaa
Watanzania na inayoakisi maoni yao kama yalivyowasilishwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba.
Amvaa Sitta
“Samuel Sitta asiendelee kuwachezea Watanzania,
kwani yeye ni mtu gani huyo? Yuko juu ya nani? Anaogopeka na nani?
Namwambia Sitta endapo atasababisha vurugu yoyote baada ya maafikiano
tuliyofikia na Mheshimiwa Rais, endapo damu yoyote itamwagika kwa sababu
ya ubabe wake, itabidi alipe usaliti huo.
“Wasije wakaona yanayotokea Kenya…Sitta chochote
kitakachotokea watakuja kumkamata na kumpeleka The Heague (Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai) … ole wake machafuko yoyote yatokee.”
Profesa Lipumba
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba
alisema hakukuwa na sababu kwa Bunge Maalumu kuongeza siku 60 kwa kuwa
hakukuwapo na maridhiano ya vyama vya siasa wakati uamuzi huo
ulipochukuliwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Alisema hatua ya kuliongezea muda Bunge hilo,
imelisababishia Taifa hasara kubwa na kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti wa
Hesabu za Serikali (CAG) kukagua hesabu za fedha zilizotumika
“Tunasikia walikuwa wanakunywa chai ya asubuhi na jioni ya
Sh10,000 na chakula cha mchana Sh25,000 hata wajumbe ambao hawapo
wanalipiwa… hata wakati tunajadili Katiba, mambo ya msingi ya uwazi,
uwajibikaji na uadilifu waliyakataa yasiwemo ndani ya tunu za Taifa,”
alisema Profesa Lipumba.
Dk Willibrod Slaa
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema
amebaini kuwa siku 60 za kwanza hazikuwekwa na Sheria, bali zilitolewa
kama Tangazo la Serikali (GN) ambayo ni taarifa inayotangazwa katika
gazeti la Serikali na Rais na Waziri.
Hivyo alisema, Rais angeweza kuliahirisha wakati
wowote kwa kuwa kauli yake haikuwa sheria kama ambavyo amenukuliwa
akisema mara kwa mara kuwa sheria inambana kuliahirisha.
“Rais alipaswa kwenda tena kwenye Gazeti la
Serikali kufuta tangazo lake, haihitaji kwenda kwa wabunge, hahitaji
kupiga magoti, hahitaji kubembeleza mtu, ni utashi wa Rais mwenyewe,”
alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Anaogopa kuchukua hatua kwa sababu wale
watalalamika, maana yake Rais anajali zaidi malalamiko ya watu 600
kuliko malalamiko ya Watanzania milioni 40 ambao hawana mlo wa siku,”
alisema.
Alisema pamoja na makubaliano waliyofikia kati ya
vyama vya siasa na Rais Kikwete, bado Sitta ameendelea kuwahadaa
wananchi kuwa Katiba Mpya itapatikana kabla ya Oktoba 4, mwaka huu.
Freeman Mbowe
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Baraza la
Vijana wa Chadema, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema
Ukawa hawako tayari kuona Bunge hilo likiendelea na vikao vyake hadi
Oktoba 4, mwaka huu.
“Hatuwezi kukubali ubadhirifu wa fedha unaoendelea
Dodoma hadi Oktoba 4, tutawaeleza vijana wetu tuingie barabarani, kwani
tumechoshwa na dhuluma zinazofanywa na CCM na Serikali yake,” alisema
na kuongeza:
“Kama Rais anashindwa kuzuia ubadhirifu wa fedha
unaoendelea Dodoma eti kwa sababu sheria haimruhusu na kuwaacha
waendelee kwa wiki tatu zaidi, hatuwezi kukubali tutakutana barabarani.”
Mbowe alisema wamevumilia vya kutosha na kuwapa
nafasi ya kutafakari lakini wamewapuuza, jambo ambalo wameeleza
hawatalikubali liendelee.
“Katika uchaguzi ngazi ya Taifa Chadema, (Septemba 14), kutakuwa na
wajumbe mbalimbali kutoka Ukawa, nitatumia hadhara hiyo kuwaeleza ni
lini vijana wetu tutaingia barabarani.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment