Thursday, January 01, 2015
ZITTO: NITAMUUNGA MKONO MBOWE
HAKI SAWA: Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) na
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe
wakiwasili kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana, ambako
walihutubia mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe pale atakapowasilisha
hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni katika mradi
wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Zitto aliyasema hayo jana katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mkoani hapa uliandaliwa na
Chama cha Wananchi (CUF) kuwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kuwachagua
viongozi wa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Najua bado mnalia kuhusu bomba la kupeleka gesi
Dar es Salaam, machozi yenu yatafutika kwani tayari habari za ufisadi
mkubwa katika ujenzi wa bomba hili zimeanza kuchomoza. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
WATU 20 WAFARIKI HARUSINI
Sherehe
moja ya harusi nchini Afghanistan, imeshambuliwa kwa mzinga uliorushwa
na roketi na kusababisha mauaji ya watu 20 na kuwajeruhi wengine zaidi
ya kumi na mbili.
Kisa hicho kilitokea wakati wa makabiliano
makali kati ya walinda usalama wa Afghanistan na wapiganaji wa Taliban
katika jimbo la Helmand.
Mmiliki wa jumba lilofanyiwa harusi hiyo
amesema kuwa wageni walikuwa wanajikusanya nje kumkaribisha bi harusi,na
kuongezea kuwa watoto wake tisa wametoweka.
Waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya Lashkar Gah,mji mkuu wa mkoa huo.
Shambulio
hilo limetokea wakati wa siku ya mwisho kwa ujumbe wa wanajeshi wa
Marekani na wale wa shirika la kujihami la NATO wanaoondoka nchini
Afghanistan. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
PAPA AKEMEA UFISADI MWAKA MPYA
Papa
Francis ametumia sherehe za kuupokea mwaka wa 2015 kuzungumzia tatizo
la rushwa katika mji wa nyumbani wa Rome nchini Italia.
Akizungumza
katika Kanisa kuu la St. Peter Basilica, papa amesema rushwa ni
shumbulizi dhidi ya maskini na wasiokuwa na uwezo ambapo ametaka
mabadiliko ya kiroho na kimaadili katika mji huo.Papa ambaye ndiye Askofu wa Rome amefanya utetezi dhidi ya maskini kama nguzo muhimu katika uongozi wake wa upapa.
Maafisa wa polisi kwa sasa wanawachunguza maafisa wa Roma wanaotuhumiwa kujihusisha na kundi la Mafia na ufisadi dhidi ya fedha za umma zikiwemo zilizotengwa kwa ajili ya kituo wahamiaji. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
MWAKA MPYA MAAAFA CHINA WATU 35 WAFARIKI
Sherehe
za kuupokea mwaka mpya 2015 zimeguka kuwa majonzi baada ya watu
thelathini na watano kufa kwenye taharuki ya kukanyagana kwenye
msongamano wakati wakiiupokea mwaka mpya.
Maafa hayo yametokea katika mji Shanghai ambapo maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika ili kuupokea mwaka mpya.Chanzo cha taharuki hiyo bado haijafamika lakini vyombo vya habari vya nchi hiyo vimenukuliwa vikisema imetokana na maelfu ya watu kuzuiwa kugombea fedha bandia zilizotupwa eneo hilo kutoka katika jengo moja. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
KANO WAPOKEA MWAKA MPYA MARA YA KWANZA
Mwaka mpya wa 2015 umepokewa kwa kishindo katika maeneo mbali mbali duniani na barani Afrika.
Nchini
Nigeria kumekuwa shamra shamra ambapo kwa mara ya kwanza mafataki
yalirushwa katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo lenye waislamu wengi.Shamra shamra hizo zimefanyika katika kituo cha michezo katika mji wa Kano ambapo waliohudhuria ni wale waliopata mwaliko pekee.
Habari zinasema kumekuwa na mwitikio mkubwa ambapo umati wa watu ulihudhuria shamra shamra hizo jambo lililowapa wakati mgumu maafisa usalama kuudhibiti umati huo.
Waandaji wa shamra shamra hizo za maonyesho ya kulipua mafataki hayo wanasema wanataka jimbo la Kano kuungana na miji mingine mikubwa duniani kusherehekea siku kuu ya Mwaka Mpya.
Ulinzi mkali uliimarishwa kwa tahadhari ya shambulio lolote kutoka kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC
RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND LEO, MAN U, ARSENAL, CHELSEA MZIGONI
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz. |
---|
England – Premier League | ||||
---|---|---|---|---|
15:45 | Stoke City | ? – ? | Manchester United | |
18:00 | Aston Villa | ? – ? | Crystal Palace | |
18:00 | Hull City | ? – ? | Everton | |
18:00 | Liverpool | ? – ? | Leicester City | |
18:00 | Manchester City | ? – ? | Sunderland | |
18:00 | Newcastle United | ? – ? | Burnley | |
18:00 | Queens Park Rangers | ? – ? | Swansea City | |
18:00 | Southampton | ? – ? | Arsenal | |
18:00 | West Ham United | ? – ? | West Bromwich Albion | |
20:30 | Tottenham Hotspur | ? – ? | Chelsea |
KOMBE LA MAPINDUZI KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO
MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inaanza kutimua vumbi leo Visiwani
Zanzibar ambapo Simba itacheza na Mtibwa Sugar, na mabingwa watetezi,
Azam watacheza na KCCA ya Uganda Ijumaa kwenye Uwanja wa Amaan.
Mashindano hayo ni maalumu kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Mapinduzi
ya Zanzibar yanashirikisha timu mbalimbali kutoka ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati ambazo ni KCCA, Sports Club Villa zote kutoka Uganda,
El Merreikh ya Sudan, Ulinzi ya Kenya, Azam, Simba na Yanga zote kutoka
Tanzania Bara na Shaba, JKU, Mtendeni, Mafunzo na KMKM kutoka Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo ambao
ni Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) zilisema kwamba baadhi ya timu
zimeshawasili kwa ajili ya mashindano hayo.
Michuano ya mwaka huu inatarajia kuwa na ushindani mkali kutokana na
kushirikisha timu nyingi kubwa na zinazofahamiana kutoka ukanda huu wa
Afrika Mashariki na Kati. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
WILFIED BONY AWINDWA NA MAN CITY
Wilfried Bony anawindwa na Manchester City
Manchester
City wameanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Swansea City,
Wilfried Bony kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 25.
Mwenyekiti
wa Swansea, Huw Jenkins alisema jana kuwa klabu yake haijapokea ofa
yoyote mpaka sasa, lakini City wameshafungua mazungumzo ili kumnasa
Muivory Coast huyo ambaye pia anawaniwa na Real Madrid.
Mazungumzo yalifanyika na washauri wa Bony jana usiku.
Wiki ijayo Bony ataenda Abu Dhabi ambapo Ivory Coast imeweka kambi ya kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika mwaka huu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Wednesday, December 31, 2014
CCM KUTUMIA PANGA LA 2005
Vigezo 13 vilivyowekwa na CCM
katika Uchaguzi Mkuu wa 2005 kumpima mwanachama anayefaa kugombea urais,
ndivyo vitakavyotumika kuwaengua makada wanaoendelea kujitokeza kuwania
nafasi hiyo mwakani, imefahamika.
Vigezo hivyo vinaonekana kuwa kizingiti kwa baadhi
ya makada wa chama hicho ambao tayari wametangaza na wengine wanaotajwa
kutaka nafasi hiyo ya juu nchini, ukiachilia mbali mnyukano
unaotarajiwa kutoka vyama vya upinzani vinavyoonekana kupata nguvu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula
amelithibitishia gazeti hili kwamba, “Sifa hizo 13 zilizotumika mwaka
2005 na 2010 ndizo zitakazotumika pia mwaka 2015 na wala hakutakuwa na
maboresho wala nyongeza ya aina yoyote.”
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
ASKOFU MKUDE AASA VIONGOZI KUWA WAADILIFU
Askofu Telesphor Mkude wa Kanisa
Katoliki Jimbo la Morogoro
WATUMISHI wa umma wa ngazi mbalimbali waliopewa dhamana ya
kuwatumikia wananchi wameombwa kuzisoma na kusikiliza kwa umakini hotuba
mbalimbali za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili
ziwaweke kwenye msingi wa kuwa na maadili mema, uadilifu na uwazi.
Changamoto hiyo imetolewa na Askofu Telesphor Mkude wa Kanisa
Katoliki Jimbo la Morogoro, hivi karibuni wakati akizungumza na gazeti
hili kwenye ofisi ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrice, mjini Morogoro.
Akijikita katika suala la maadili ya viongozi wa umma, Askofu Mkude,
alisema suala la kufuata maadili, kuonesha uadilifu na uwazi katika
uwajibikaji wa kuwatumikia wananchi ni sifa kuu ya kiongozi yoyote yule.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
RAIS JAMMEH "BADO NIPO MADALAKANI"
Rais
wa Gambia amesema kuwa bado analiongoza taifa hilo la Afrika magharibi
baada ya vikosi vyake vya usalama kutibua jaribio la mapinduzi.
Yahya Jammeh amesema kuwa kamanda mmoja wa jeshi wa zamani alijaribu kuchukua udhibiti wa taifa hilo alipokuwa ziarani Ufaransa.Hatahivyo hajulikani aliko.Milio mikali ya riasi ilizuka karibu na makao ya rais katika mji mkuu.
Bwana Jammeh alichukua mamlaka kupitia mapinduzi mwaka 1994 na wapinzani wake wamekuwa wakimkosoa kwa uongozi wake wa kiimla.
Duru za kidiplomasia na zile za kijeshi zinasema kuwa wanajeshi kutoka kwa jeshi la ulinzi wa rais wanadaiwa kufanya shambulizi hilo katika makao ya rais mjini Banjul mapema siku ya jummane.
Serikali imekana kwamba kulikuwa na jaribio la mapinduzi katika taarifa iliotangazwa katika radio ya taifa.
Hatahivyo,bwana Jammeh baadaye alikiri kuhusu shambulizi hilo na kusema kuwa wanajeshi waaminifu wa Lamin Sanneh aliyemtaja kama mwenye aibu walivamia mji mkuu wa Gambia kutoka Senegal katika jaribio la kutaka kuipindua serikali yake.
Amesema kuwa wavamizi hao hatahivyo walikabiliwa na vikosi vya usalama na kuwaua wanne kati yao huku wengine wanne zaidi wakikamatwa. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
RAIS MPYA WA TUNISIA KUAPISHWA
Rais mteule wa Tunisia Beji Caid Essebsi anatarajiwa kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza uliokuwa huru nchini humo. Alimshinda rais aliyekuwa mamlakani Moncef Marzouk. Ushindi wake unaaminisha kwamba Tunisia ndilo taifa ambalo limejinasua kutoka utawala wa kiimla hadi ule wa kidemokrasia.
Siku ya jumatatu,tume ya uchaguzi ilithibitisha kuwa bwana Essebsi alishinda kura ya raundi ya pili dhidi ya Marzouk. Rais huye mteule ataapishwa katika bunge la wawakilishi wapwa ambapo chama chake Nidaa Tounes kimepata wabunge wengi.
Tayari maandalizi ya kumuapisha yamekamilika mjini Tunis.
Hatua hiyo hiyo itafikisha tamati mvutano wa demokrasia wa miaka minne ya ghasia zilizoghubika taifa hilo zilizopeleekea kung'olewa kwa utawala wa Rais Zine el-Abedine Ben Ali.
Bwana Essebsi alihudumu katika utawala wa Ben Ali, pamoja na uongozi wa rais wa zamani Habib Bourguiba. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Siku ya jumatatu,tume ya uchaguzi ilithibitisha kuwa bwana Essebsi alishinda kura ya raundi ya pili dhidi ya Marzouk. Rais huye mteule ataapishwa katika bunge la wawakilishi wapwa ambapo chama chake Nidaa Tounes kimepata wabunge wengi.
Tayari maandalizi ya kumuapisha yamekamilika mjini Tunis.
Hatua hiyo hiyo itafikisha tamati mvutano wa demokrasia wa miaka minne ya ghasia zilizoghubika taifa hilo zilizopeleekea kung'olewa kwa utawala wa Rais Zine el-Abedine Ben Ali.
Bwana Essebsi alihudumu katika utawala wa Ben Ali, pamoja na uongozi wa rais wa zamani Habib Bourguiba. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
BOKO HARAM WAVAMIA KIJIJI NA KUUA WATU 15
Wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15.
Shambulizi
hilo lilitokea katika kijiji cha Kautikari katika jimbo la Borno, pale
washukiwa wa Boko Haram walipowasili kijijini humo kwa magari yenye
silaha, wakilenga askari wa ulinzi wa jadi wa mji huo.Kijiji hicho kipo karibu na Chibok mahali ambapo kundi la Boko Haram, liliwateka nyara wasichana wa shule zaidi ya mia mbili mwezi Aprili mwaka huu.
Zaidi ya watu elfu kumi wameuwawa Nchini Nigeria na Boko Haram mwaka huu pekee. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Subscribe to:
Posts (Atom)