Thursday, January 01, 2015

KOMBE LA MAPINDUZI KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO

MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inaanza kutimua vumbi leo Visiwani Zanzibar ambapo Simba itacheza na Mtibwa Sugar, na mabingwa watetezi, Azam watacheza na KCCA ya Uganda Ijumaa kwenye Uwanja wa Amaan.
Mashindano hayo ni maalumu kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Mapinduzi ya Zanzibar yanashirikisha timu mbalimbali kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambazo ni KCCA, Sports Club Villa zote kutoka Uganda, El Merreikh ya Sudan, Ulinzi ya Kenya, Azam, Simba na Yanga zote kutoka Tanzania Bara na Shaba, JKU, Mtendeni, Mafunzo na KMKM kutoka Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo ambao ni Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) zilisema kwamba baadhi ya timu zimeshawasili kwa ajili ya mashindano hayo.
Michuano ya mwaka huu inatarajia kuwa na ushindani mkali kutokana na kushirikisha timu nyingi kubwa na zinazofahamiana kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Mechi nyingine ya ufunguzi ambayo kama ilivyo kwa mechi ya Azam na KCCA inayotarajiwa kuvuta hisia kubwa za mashabiki ni baina ya Simba na Mtibwa Sugar zote za Tanzania Bara.
Mtibwa wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara tangu kuanza kwa ligi hiyo, huku Simba yenyewe ikishika nafasi 10 na matokeo ya mwisho baina ya timu hizo Mtibwa Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Azam Chamazi.
Kwenye mechi ya ligi timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 kwa Simba kutangulia kwa bao la Joseph Owino kabla ya Mussa Mgosi kuisawazishia Mtibwa Sugar kwenye kipindi cha pili.
KCCA ambayo ni bingwa mtetezi wa mashindano hayo itacheza na Azam mechi itakayorudisha hisia za mashabiki wa timu hizo mbili nyuma kwani zilikutana nchini Uganda kwenye mchezo wa kirafiki na wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Ni wazi kutokana na matokeo hayo ingawa ni ya mechi ya kirafiki Azam itataka kulipa kisasi, huku KCCA kwa upande wao wakitaka
kuendeleza ushindi.
Ofisa Habari wa Azam Fc, Jaffery Iddi alisema kwamba wanatoa umuhimu mkubwa kwa mechi hiyo na mashindano hayo kwa ujumla
kwani ni muhimu katika maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa mwaka huu.
Alisema kuwa kupangwa kukutana na KCCA ya Uganda ni kitu kilichowafurahisha kwani kitatoa fursa kwa kocha wao Joseph Omog
kulipa kisasi cha kufungwa na timu hiyo nchini Uganda kwenye mechi ya kirafiki. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...