Thursday, January 01, 2015

MUUMINI MBARONI KWA KUFANYA FUJO KANISANI

Leonard Paul
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo
POLISI mkoani Morogoro linamshikilia Jackson Mnyilemi (20), ambaye ni muumini wa Kanisa la Moravian Tarafa ya Malinyi wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuhusika kufanya fujo kanisani.
Fujo hizo zilisababisha kujeruhiwa kwa waumini wawili kwa kukatwa sehemu za usoni na mikononi na kitu chenye ncha kali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema jana kuwa tukio hilo ni la Desemba 28, 2014 majira ya saa 10 : 40 asubuhi katika kijiji cha Makelele na kuwataja waumini waliojeruhiwa kuwa ni Maria Silumbwe (47) na Aron Silumbwe (20), wote wakazi wa Kijiji hicho kilichopo Tarafa ya Malinyi wilayani Ulanga. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, tukio hilo lilitokea wakati waumini wa kanisa hilo wanaingia kanisani na ndipo kundi la mzee Anthony Mnyilemi (53), mkazi wa Makelele ambaye ni Mwenyekiti wa Kanisa hilo, alipowanyang’anya ngoma wanakwaya wa kanisa hilo na kusababisha kutokea kwa fujo.
Kamanda alisema chanzo cha vurugu hizo ni mgogoro wa uongozi wa kanisa hilo, ambao baadhi ya waumini hawamtaki mchungaji mpya aliyetoka mkoani Mbeya, Johnson Silumbwe (50) ambaye mkazi wa Makelele katika Tarafa hiyo ya Malinyi.
Alisema kutokana na vurugu hizo, mtu mmoja, Jackson Mnyilemi (20), ambaye ni mkazi wa kijiji hicho anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na fujo hizo na watuhumiwa wengine wametoroka na wanatafutwa ili watiwe mbaroni na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, waliojeruhiwa wanadhaniwa miongoni mwa familia ya na mchungaji mpya Silumbwe. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...