Leo
ni miaka 99 tangu kuanzishwa kwa siku ya wanawake duniani
iliyoadhimishwa kwa mara ya kwanza March 8, 1914 ambapo mwanzoni ilikuwa
ikijulikana kama ‘Siku ya wanawake wafanyao kazi duniani’.
Ni siku ya kuwapa heshima wanawake, kuwapongeza na kuwaonesha upendo katika jitihada zao kiuchumi, kiasiasa na kijamii.
Katika nchi zingine siku hii
imefunika ile ladha ya kuchanganyika na siasa na kuwa siku ya wanaume
kuelezea upendo wao wanawake kama ilivyo Mother’s Day na Valentine’s
Day. Soma jinsi watu mbalimbali mashuhuri nchini (na kwingineko)
wanavyoizungumzia siku hii.
Mama Salma Kikwete
Leo ni siku ya wanawake
Duniani.,ni siku ya kujitazama kama Taifa juu ya hali ya wazazi hawa na
walezi wa Taifa hili. Ni siku ya kujipima na kutathimini namna gani,
wanawake wamewezeshwa kujitambua na kushirikishwa katika mipango ya
maendeleo ya jamii yetu. Tunapofikiri kama Taifa ni namna gani tunaweza
kujikomboa katika Umasikini tulionao ni lazima mipango hiyo iende
sambamba na mipango na mikakati ya ukombozi kwa wanawake wa Taifa hili.
Nancy Sumari
Even when we are a mess, we still
put on vests with ‘S’ on our chests, Oh yes, we are Super Women, and
today is our day…Happy Womens day!!
Diamond
HAPPY WOMEN’S DAY……. I LOVE MY
MAMA MORE THAN ANYTHING IN THIS WORLD….SHE HAS BEEN THROUGH ALOT WITH
ME…… MUCH LOVE TO ALL WOMEN’S IN THIS WORLD…..!!