Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Narunyu, Kata
ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika
kijiji hicho leo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiwasalimiana na watoto wa kijiji cha Narunyu, Kata
ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika
kijiji hicho leo.
Mkazi wa Kijiji cha Ng'apa wilaya ya Lindi mjini,
akionyesha kadi yake ya matibabu ya Huduma ya Kadi ulkiopo chini ya Bima
ya Afya, wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika
kijiji hicho, leo Feb 16, 2013. Mama Salma Kikwete alimpatia fursa ya
kuzungumza wakati akihimiza umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo
wa matibabu.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akiwa amegoma kushuka katika gari lake, kukataa
kwenda kwenye mkutano wa ndani wa Chama Kata ya Tandangongoro, uliokuwa
umepangwa na viongozi wa kata hiyo kufanyika katika chumba cha darasa la
shule ya msingi ya kijiji cha Ng'apa, mkoani Lindi, leo Februari 16,
2013. Hatua hiyo iliwalazimu viongozi kutafuta ukumbi mwingine wa
dharura. Mama Salma alisema si sahihi mkutano wa ndani wa Chama cha
siasa kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya serikali
Umati wa wananchi wa Kijiji cha Ng'apa wakimsiliza
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akilipowahutubia mkutano wa hadhara leo. PICHA ZOTE NA BASHIR
NKOROMO.
No comments:
Post a Comment