Mahakama
Kuu nchini Kenya imemsafishia njia mmoja kati ya wagombea urais Bw.
Uhuru Kenyata kuwania kiti cha urais wa taifa hilo katika uchaguzi mkuu
ujao pamoja na kukabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Ikiwa
imebakia muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa Machi 4 mwaka, uamuzi huo
umemuweka Kenyatta huru kuwania kiti hicho akionekana kama mmoja kati
ya viongozi wanaongoza katika kinyang’anyiro cha urais.
Jopo
la majaji watano waliokuwa wanasikiliza kesi hiyo wanasema mahakama kuu
ndiyo yenye uwezo wa kuamua kesi hiyo.
Kesi
hiyo ilifunguliwa kupinga ushiriki wa watu hao katika uchaguzi wa mwezi
Machi, kwa kile walichokiita kukosa uadilifu kwa sababu tayari
wamefunguliwa mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa
mwaka 2007 katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC.
No comments:
Post a Comment