Rais
Idriss Deby wa Chad amewafukuza kazi mawaziri wawili wanaohusika na
masuala ya ulinzi ikiwa ni baada ya wiki iliyopita kuwasimamisha kazi
takriban polisi zaidi ya 6,000 kwa tuhuma za rushwa, upendeleo na
udhalilishaji.
Katika
tangazo lililotolewa katika radio ya taifa, rais Deby amemfukuza Waziri
wa Usalama wa Umma Ahmat Mahamat Bachir na Waziri wa Usimamizi dhidi ya
Ugaidi Bachar Ali Souleymane.
Kufukuzwa
kwa mawaziri hao kunafuatia pia kufukuzwa kazi kwa Mkuu wa Polisi
nchini humo, ikiwa ni siku mbili baada ya kulisimamisha kazi jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment