Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki akimvalisha sare za
shule na viatu mwananfunzi wa shule ya msingi Kiromo zilizotolewa na
Kampuni ya simu ya Airtel mwishoni mwa wiki hii.Airtel metoa msaada wa
sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu
728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi
Kiromo.
Meneja wa
uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi sare
za shule Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiromo Nasib Pangahela
mwishoni mwa wiki hii, akishuhudiwa na meneja wa huduma kwa jamii
(katikati) bi Hawa Bayumi.
Meneja wa
uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi mmoja
wa wanafunzi wa shule ya msingi Kiromo sare za shule zilizotolewa na
Kampuni ya simu ya Airtel mwishoni mwa wiki hii, akishuhudia
makabidhiano hayo (wa pili kushoto) meneja wa huduma kwa jamii bi Hawa
Bayumi akifuatiwa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiromo Nasib
Pangahela, Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 ,
skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi
milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.
Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki (Kulia)
akimpongeza Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kiromo (kulia) baada ya
makabidhiano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii wakishuhudiwa na meneja
wa huduma kwa jamii wa Airtel Hawa Bayumi (wa pili kulia) akifuatiwa na
mmoja wa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo bi Zuwena Salumu, Airtel
metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati
1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule
ya msingi Kiromo.
Airtel
Tanzania yatembelea shule ya Kiromo mwishoni mwa wiki hii na kukabidhi
sare za shule pamoja na viatu vyenye dhamani ya shilling milioni 50.
Katika msaada huo Airtel imetoa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 ,
skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728, hafla ya makabidhiano ilifanyika
katika shule hiyo iliyopo Kiromo -Bagamoyo.
*** ***
Alhamisi
10 February 2013, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa gharama
nafuu zaidi Tanzania, leo imegawa sare za shule pamoja viatu katika
shule ya msingi Kiromo iliyopo Bagamoyo ikiwa ni sehumu ya shughuli zao
za kusaidia jamii.
Shule ya kiromo ni moja kati ya shule zilizofaidika na mpango wa shule yetu na kuingia kwenye ukarabati wa majengo na madarasa na kubadili mazingira ya shule na kutoa vifaa vya kufundishia pamoja na computer. sasa Airtel imetoa Sare na viatu vya shule kwa wanafunzi wote shuleni hapo.
Katika kauli iliyotoleawa na kampuni ya Airtel Tanzania kupitia Meneja shughuli za kijamii bi. Hawa Bayumi alisema” Airtel imedhamiria kuendelea kuisadia shule mbalimbali kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwepo vya kufundishia ili kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Na leo tunaendelea kuboresha shule yetu ya Kiromo kwa kutoa msaada wa uniform na viatu kwa wanafunzi.
M msaada wa
sare zashule tunazoto ni pamoja na Kaptura 600 , skirt 600 , mashati
1193 na viatu 728 vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya
msingi Kiromo.
Airtel Tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka na upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
Leo
tunathibitisha dhamira yetu ya kusaidia mashule kwa kutoa sare za shule
na viatu Kiromo shule ya msingi”, alisema Bayumi Airtel itaendelea
kusaidia mashule kwa kutoa vitabu na vifaa mbali mbali vya kufundishia
ikiwa ni sehemu ya shughuli zetu za kusaidia jamii, nia yetu ni
kuwafikia shule nyingi zaidi katika mikoa yote ya Tanzania aliongeza.
Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini. Tangu tulipoanza mradi wa “ shule yetu” mpango wa kusaidia vitabu na vifaa vya shule , shule mbalimbali nchini zimeshafaidika na mradi huu mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment