Mshitakiwa
wa kwanza katika kesi ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la
Iramba Magharibi Mwita Waitara Mwakibe akitoka nje ya mahakama ya hakimu
mkazi mjini Singida baada ya kesi yao kuahirishwa leo, Kesi hiyo
imeahirishwa hadi Machi 11 mwaka huu,baada ya mashahidi wa upande wa
mashitaka kuingia mitini.
Wakili
wa washitakiwa vigogo wa CHADEMA Onesmo Kyauke (katikati) akiwaeleza
jambo wateja wake muda mfupi baada kesi ya wateja wake kuahirishwa hadi
Machi 11 mwaka huu.Vigogo hao wanaoshitakiwa kwa kumtolea lugha ya
matusi mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mwigullu Lameck Nchemba.
Dk.Kitila Mkumbo (kushoto) na afisa sera na utafiti, Mwita Waitara
Mwakibe (kulia).(Picha na Nathaniel Limu).
Mashahidi
watano wa upande wa mashitaka yanayowakabili vigogo wawili wa CHADEMA
taifa, wameingia mitini na kusababisha kesi kuahirishwa kusikilizwa hadi
Machi 11 mwaka huu.
Mashahidi
hao walikuwa watoe ushahidi dhidi ya washitakiwa Afisa Sera na Utafiti
wa CHEDEMA Makao Makuu Mwita Waitara Mwikwabe (37) na Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Dar-es-salaam na Mshauri wa CHADEMA Dk.Kitila Mkumbo.
Vigogo
hao wanatuhumiwa kutoa lugha ya matusi kwa mbunge wa jimbo la Iramba
magharibi Mwigullu Lameck Nchemba.
Mwendesha
mashitaka mwanasheria wa serikali Mary Mudulugu amedai mbele ya hakimu
mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida Rusth Massam, kuwa
askari polisi ambaye ni mpelelezi wa kesi hiyo yupo Dar-es-salaam
kitendo kilichopelekea mawasiliano baina yao,yakatike.
Amesema
kutokana na mpelelezi huyo kuwa jijini Dar-es-salaam, mawasiliano na
mashahidi hao watano ambao ni wa mwisho katika kesi hiyo,yamekuwa magumu
na yamesababisha washindwe kufika mahakamani.
Kabla
ya kuahirishwa kwa kesi hiyo,wakili wa washitakiwa Onesmo Kyauke,
aliiomba mahakama hiyo kutaja tarehe ya mwisho kwa upande wa mashitaka
kuleta mashahidi wao na endapo watashindwa kuwaleta, mahakama ifunge
ushahidi kwa upande wa mashitaka.
No comments:
Post a Comment