Monday, February 11, 2013

Chris Brown anusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari akiwakimbia Paparazzi

Muimbaji machachari wa Marekani Chris Brown amenusurika baada ya kugonga gari yake katika ukuta akidai alikuwa akifuatwa na mapaparazzi .
Polisi mjini Beverly Hills wamesema mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye katika ajali hiyo hakujeruhiwa, alishindwa kulimudu gari lake aina ya Porsche Turbo Nyeusi  alipokuwa ajaribu kuwatoroka.
Taarifa zinasema Brown alikuwa akiendesha gari hilo mwenyewe na aligonga ukuta.
Ajali hiyo imetokea siku moja kabla ya kutolewa kwa tuzo za Grammy huko LA’s Staples Center ambapo alikuwa mmoja wa wagombea.
Mapema wiki iliyopita rekodi za kimahakama zilidai kuwa  mwezi uliopita Chris Brown alimtishia kumpiga risasi muimbaji Frank Ocean  wakati wa mapambano ya kugombea sehemu ya kuegesha gari.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...