Monday, July 22, 2013

MIILI YA ASKARI WA JWTZ WALIOUAWA DARFUR KUAGWA LEO MAKAO MAKUU YA JESHI

 
Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanatarajiwa kuagwa leo kwenye viwanja vya makao makuu ya jeshi hilo.
Miili ya wanajeshi hao iliwasili nchini juzi kwa ndege maalumu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J. K Nyerere, Terminal One na kwenda kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
 
Wanajeshi waliouawa ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Rodney Ndunguru, Peter Werema na Fortunatus Msofe.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya JWTZ, ilieleza kuwa askari hao wataagwa leo na shughuli hiyo itahudhuriwa na familia, makamanda wa jeshi na viongozi wa Serikali.

LOWASSA, DK. SLAA, MEMBE WAWEKWA NJIA PANDA KUWANIA URAIS.....!!!

*Rasimu kutumika kuwaondolea sifa ya kugombea urais
*Yumo pia Membe, Magufuli, Sitta, Zitto na Wassira


Freeman Mbowe

Dk. Wilbrod Slaa
MKAKATI wa kuwaengua vigogo wanaotajwa kung’ang’ania kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 sasa umebainika, MTANZANIA Jumapili linaripoti.

 Kwa mujibu wa uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili,    mkakati huo ambao umelenga kuwang’oa viongozi hao,  unadaiwa kutekelezwa na baadhi ya wanasiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Rasimu ya Katiba Mpya, iliyotolewa hivi karibuni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.



Dk. Emmanuel Nchimbi


Steven Wassira
Imeelezwa kuwa kupitia Rasimu hiyo ya Katiba Mpya, kuna vipengele vilivyopenyezwa kwa nia ya kuwabana watu fulani fulani ndani na nje ya CCM ambao wanatajwa kuusaka ukuu wa dola mwaka 2015 na chama hicho hakitaki kuona wanakuwa kikwazo dhidi yake.

Mtoa habari wetu ndani ya CCM alilidokeza gazeti hili kuwa vipengele hivyo ambavyo vimewekwa kama mtego, ni vile vinavyotaja sifa za mgombea Urais na mgombea Ubunge.


January Makamba


Bernard Membe
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, kutokana na hilo, baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM kwa makusudi wameamua kuufanya mjadala kuhusu serikali tatu kuwa mkali, ili kuzuia mjadala mpana katika masuala mengine.

Kipengele ambacho kama kikiachwa bila kufanyiwa marekebisho kinaweza kuwabana wanasiasa wengi ndani na nje ya CCM wanaotajwa kuwania Urais 2015 ni pamoja na kile cha Sura ya Saba, ambacho kinazungumzia Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu Serikali, Rais na Makamu wa Rais, katika sehemu ya kwanza C kwenye kipengele cha 75 (E) kinachozungumzia sifa za Rais kimeeleza kuwa mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa: anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hiyo.

SAMAKI WALIOVULIWA KWA MABOMU NA SUMU WATAPAKAA KWENYE MASOKO JIJINI DAR ES SALAAM


Wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wameambiwa wachukue tahadhari na umakini wakati wa kununua samaki nyakati za jioni, kutokana na madai kuwa baadhi ya wachuuzi huvua kwa kutumia mabomu.

Tahadhari hiyo imekuja baada ya kufanya uchunguzi wa muda mrefu, ambapo imegundua samaki hao wanauzwa nyakati hizo kukwepa kugundulika.
Imefahamika licha ya Serikali kuwa na kampeni ya kusaka watu wanaojihusisha na uvuvi huo, bado hali imekuwa mbaya katika maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi.


Maeneo yanayotajwa kukithiri kwa uvuvi wa mabomu ni Pwani ya Bagamoyo, Kawe katika Manispaa ya Kinondoni na Buyuni eneo la Kigamboni, Manispaa ya Temeke.

Baadhi ya wavuvi waliofanikiwa kuzungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa usalama, walisema watu wanaojihusisha na uvuvi haramu wanatumia mbinu nyingi za kuingiza samaki sokoni.
Walisema watu wengi kutokana na kuanza kuwabaini samaki wa aina hiyo, wavuvi wanawauza kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu nyakati za jioni bila ya kugundulika kwa urahisi.

Sunday, July 21, 2013

STORY KUHUSU LINAH KUBAKWA, MWENYEWE AFUNGUKA AELEZA KILA KITU, MSIKILIZE HAPA....!!!

Linah akiwa katika pozi kali.

Mrembo na mwanamuziki wa kike nchini, Linah Sanga amezikanusha ripoti zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na rapper Kimbunga na kudai kuwa ameshangazwa mno na taarifa hizo. Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo mchana baada ya akaunti ya Facebook inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha Mizinga’ kuandika:
“Mtoto kimbunga amechamba ana leta usela mavi mambo ya kizamani hivi yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa kosa la kumbaka msanii lina.”
Bongo5 imezungumza na Linah ambaye amesema amepigiwa simu na watu wengi wa karibu kumuuliza suala hilo wakiwemo, Barnaba, Ditto, Amini na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown.
 

Amesema Soudy alimwambia kuwa ameziona taarifa hizo kwenye Facebook kwenye akaunti ya Kalapina.

LUDOVICK AFUNGUKA AELEZEA UHUSIANO WAKE NA LWAKATARE NA MWIGULU NCHEMBA...!!!



*Aelezea uhusiano wake na Mwigulu, Lwakatare
*Asema yeye bado ni mwanachama hai wa Chadema, amkwepa Kibanda
SIKU chache baada ya Mahakama kumuachia kwa dhamana mshitakiwa mwenza wa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, Joseph Ludovick, amefunguka na kuelezea tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake, ikiwamo uhusiano wake na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba.

Ludovick, ambaye anadaiwa kurubuniwa na Nchemba na hivyo kumrekodi Lwakatare wakipanga mipango ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaky, alijitokeza juzi katika mtandao wa kijamii wa Mabadiliko na kuomba kuulizwa jambo lolote, kwa kile kilichoonekana kutaka kujibu tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yake.

Maswali na majibu yake ilikuwa ni kama ifuatavyo;

KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MWIGULU

Akielezea uhusiano wake na Mwigulu baada ya kuulizwa swali na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Abdul Dello, Ludovick alisema ni wa kawaida na kwamba haufikii kama ule wa Lwakatare na Maggid Mjengwa.

“Tumejuana kwenye mitandao ya kijamii na tukadevelop ukaribu, ilitokana na mimi kukosoa mijadala yake na kumpinga.

MAN U WAENDELEA NA MAZOEZI KATIKA UFUKWE WA BONDI


All at sea: The Manchester United squad had a training session at Bondi BeachMambo ya ufukweni: Kikosi cha Manchester United kimefanya mazoezi katika Ufukwe wa Bondi

Life's a beach: United players, left to right, Anderson, Robin van Persie, Rafael da Silva and Tom CleverleyMaisha ya bichi hayo: Wachezaji wa United , kushoto kuelekea kulia, Anderson, Robin van Persie, Rafael da Silva na Tom Cleverley 

Water a view: United manager David Moyes takes in the sights of Sydney Harbour on the way to Bondi BeachKocha wa United., David Moyes akipozi katika bandari ya  Sydney  kabla ya kupanda boti kuelekea  ufukwe wa  Bondi 

SERIKALI KUTOA UAMUZI MPYA WA SERIKALI KUHUSU KODI YA LINE....!!!


Wakati Serikali imeeleza nia yake ya kuangalia upya utozaji wa kodi ya kila mwezi kwenye laini za simu za mkononi, imeeleza pia mpango wa kufunga mtambo maalumu ili kubaini malalamiko ya kampuni za simu kudaiwa kuiba fedha za watumiaji.

Katika kile kinachoonesha kusikiliza kilio cha wananchi, Serikali imesema inapitia maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wadau ili kuiangalia upya sheria hiyo ya kutoza kodi ya Sh 1,000 kwa kila laini kwa nia ya kuwapunguzia wananchi mzigo huo.


Serikali imetoa kauli hiyo Dar es Salaam jana kupitia kwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa walipozungumza na waandishi wa habari.

SHILOLE AAHIDI KUMCHAPA SINTAH, KISA .........!!!


clip_image002 

Shilole mwigizaji wa filamu Swahiliwood.GIZAJI wa kike wa filamu na muziki Bongo zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemtangazia hali ya hatari msanii mwenzake wa filamu na mtangazaji wa televisheni Christina John ‘ Sintah’ kuwa popote atakapomkuta lazima amchape kwa kipigo ambacho hatasahau katika maisha yake, Shilole kaongea hayo kufuatia kuandikwa na mwanadada huyo katika mtandao wake akimbeza kwa kejeli.
zuwena Mohamed 
shilole akiwa Marekeni katika moja ya maduka.
“Ni kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez) kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda kufanya show Marekeni! Sasa ninachomwambia ninamtafuta nikikutana naye nimtapa kipigo cha Mbwa mwizi,” aliongea kwa hasira Shilole

IMEBAINIKA KUWA ASILIMIA 48.3 YA WANAUME TANZANIA WAMEBAMBIKIWA WATOTO NA WAKE ZAO....!!!


Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini imesema karibu nusu ya watu waliojitokeza kupima vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa watoto wao, vipimo vimeonesha si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.

Takwimu hizo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2010, ikionesha kuwa, asilimia 48.32 ya wazazi 'wanalea' watoto wasio wa kwao wakati asilimia 51.68 ndio wazazi halali.

Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Jinai, Vinasaba na Baiolojia wa ofisi hiyo, Gloria Machuve katika mkutano na wanahabari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dar es Salaam.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 21, 2013

DSC 0040 f2962

DSC 0044 11fb4

MAKUBWA ETI.... "HAKUNA MFANYABIASHARA MKUBWA NCHINI ALIYEFANIKIWA BILA KUTOA RUSHWA SERIKALINI".... REGINALD MENGI


MWENYEKITI wa kampuni za IPP, Reginald Mengi ametoboa siri kuwa hakuna mfanyabiashara wa Tanzania aliyefanikiwa katika biashara kubwa kwa kusaidiwa na serikali bila ya kutoa rushwa. 

Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), alisema yeye aligoma kutoa rushwa kwa watendaji wa serikali jambo lililosababisha kupoteza fursa nyingi ambazo zingemfanya awe na maendeleo zaidi ya aliyonayo hivi sasa.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam wakati akichangia mada katika uzinduzi wa ripoti ya uchumi na maendeleo barani Afrika kwa mwaka 2013, ...tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku upate hacari... uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Diplomasia. Alisema kutokanana na kukithiri huko kwa rushwa, maendeleo ya kibiashara na kijamii hapa nchini hayawezi kufikiwa kama jitihada za kupambana na rushwa zitapuuzwa.

Saturday, July 20, 2013

SIKILIZA WIMBO WA MZEE MAGARI...!!!


Daaaah! Mzee Magari kweli kipaji kipo hebu chukua dakika chache kusikiliza wimbo huu afu dondosha comment yako.

AJALI MBAYA: KICHWA CHA MWANAMKE CHANASA KWENYE KIOO...!!!


Wakimtoa Dereva kwanza
Wakianza kumuokoa yeye
Hatimaye ameokolewa
Mwanamke mmoja raia wa China amenusurika kifo baada ya gari aliliokuwa amepanda kupata ajali mbaya iliyomsababishia yeye kunasa kakita kioo cha Mbele maeneo ya Jimbo la Guanxi, Mwanamke huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika alikuwa kashapoteza fahamu huku damu nyingi zikimtoka katika kioo hicho.

Juhudi za ziada zilifanywa na askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji kwa kukitanua kioo hicho kwa ustaadi mkubwa huku wakihakikisha hawamkati zaidi mwanamke huyo.

KIKOSI CHA WAASI NCHINI KONGO M23 CHAWEKA PICHA YA PASSPORT YA ASKARI WA JWTZ WALIYEMKAMATA ASUBUHI YA LEO AKISHIRIKIANA NA FDLR

m23-tanzania-twitterchristopher-george-yohana 

Waasi wa M23 wa DR Congo, wanadai kuwa wamemkamata askari wa Tanzania anayeitwa Christopher George Yohana, wakati akishirikiana na waasi wa Rwanda (FDLR) wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya maelfu ya Watusi mwaka 1994.

Waasi hao wa M23 wameweka picha ya passport ya mateka huyo kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter. Kwa mujibu wa chimpreports.com,   M23 wameripoti kumkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47 yenye serial number 1372. Ifuatayo ni kauli ya M23 waliyoweka Facebook ikiambatana na picha hiyo ya Passport Juu hapo:
“Leo Fdlr zikiongozwa na askari toka Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri, walizicapa na kuzikimbiza alafu zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa cayi na mukate anywe. Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya kitu, tutamucunga muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC ambao wanatukanaka hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita, sisi ni jeshi la Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone passport ya ule askari ya tanzania ambaye tulikamata”

WASTARA JUMA .... "WANAUME WALIO MSAIDIA SAJUKI WAMENIGEUKIA NA KUNITAKA KIMAPENZI"


Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.

Bishosti huyo alisema kuwa tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa sapoti kipindi hicho, bado wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya nchi ambao wanatuma maombi kwake lakini anawaona wote ni matapeli na wanamtamani tu hivyo hayupo tayari kuingia kwenye uhusiano wa aina hiyo.

ANGALIA PICHA ZAIDI ZA MAPOKEZI YA MIILI YA MASHUJAA WA TANZANIA WALIOUAWA DARFUR ILIVYOPOKELEWA LEO JIJINI DAR




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jioni.




 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo jioni amewaongoza watanzania kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. 



Miili hiyo imewasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere – Terminal one (Air Wing) leo jioni majira ya saa kumi.

"HAKUNA UCHAGUZI WA MEYA ARUSHA" NAPE NNAUYE

Nape Nnauye
MKURUGENZI WA Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye amesema suala la uchaguzi wa Meya wa Mji wa Arusha limefikia tamati na kamwe uchaguzi huo hautafanyika tena. Nnauye alisema hayo alipozungumza na MTANZANIA jana, huku akiwataka wananchi wa Jiji la Arusha kupuuza kauli za vitisho zinazotishia kumwondoa madarakani Meya wa Jiji, Gaudence Lyimo.
Kauli ya Nnauye inafuatia kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema Arusha Isaya Doita, aliyesema kuwa ushindi wa udiwani wa chama chao katika kata nne za mji huo ni chachu katika msimamo wa chama chao kutaka uchaguzi wa Meya wa Arusha urudiwe.

Doita akiamini kuwa Lyimo alichaguliwa kwa mizengwe, alisema ana imani muda si mrefu Jiji la Arusha litapata meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria.

Hata hivyo, siku chache baadaye Katibu wa Chadema wa Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema suala la nafasi ya umeya siyo tena ajenda ya chama hicho.

Akizungumzia suala hilo jana, Nnauye alisema CCM imezoea kusikia kauli mbalimbali za vitisho zinazotolewa Chadema na kuwataka wananchi wa Arusha kuzipuuza kauli hizo.

“Ni kazi yao vitisho nia yao ni kutaka watu wasifanye shughuli zao, lakini suala la meya yupo pale na ataendelea kuwapo kwani uchaguzi ulishafanyika na hautafanyika tena.

“Kazi iliyobaki sasa kwa wananchi wa Arusha ni kujenga mji wao kwa kufanya kazi, watu wafanye kazi zao wala hakuna sababu ya kuhofia kauli za vitisho.

“Ni upuuzi kuanza kuzungumzia kila siku suala la Arusha, waliopewa dhamana wawajibike kilichobaki ni kufanya kazi, waache kusikiliza upuuzi,” alisema Nnauye.

CHANZO MTANZANIA

KOCHA MZUNGU TAIFA STARS AFARIKI DUNIA JANA

Bert Trautmann

 
Tumempoteza: Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Bert Trautmann amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89 jana.


Na Mahmoud Zubeiry na Chris Wheeler,
KOCHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na giwji wa zamani wa klabu ya Manchester City, Mjerumani Bert Trautmann amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 89.
Baada ya BIN ZUBEIRY kusoma taarifa za kifo cha kocha huyo Daily Mail, ilimpigia Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Leodegar Chilla Tenga ambaye alifundishwa na Mjerumani huyo na akasikitisha.
Tenga, ambaye sasa ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alisema kwamba Trautmann, ambaye alikuwa anasumbuliwa alikuwa mwalimu mzuri na wachezaji walimpenda sana.
Alisema kocha huyo aliyefariki asubuhi ya leo nyumbani kwake, La Losa, karibu na Valencia aliifundisha Taifa Stars kati ya mwaka 1975 na 1976.
“Alikuwa kocha mzuri, kwa sababu ni kocha aliyetokea kuwa mchezaji wa kulipwa, alikuwa anaelewa saikolojia ya wachezaji, na alikuwa mwalimu ambaye ukienda kambini unaona raha kuwa kambini.

MAAJABU:MBUZI AZALIWA NA VICHWA VIWILI TENA KWA MAUMIVU MAKALI

Kuanzia Saa 10 Alfajiri zilisikika kelele za Maumivu kutoka kwa mbuzi jike ambaye alikuwa anajifungua, Kelele zilikuwa kubwa mno kuashiria maumivu makali alikuwa anayapata kiumbe huyo, palipozidi kupambazuka ilibidi majirani waende kushuhudia kulikoni kwa mbuzi kuwa na kelele kiasi kile, na ndipo walipojionea maajabu baada ya mbuzi jike huyo kujifungua watoto watatu, wawili kati ya hao wakiwa ni wa kawaida kabisa na mmoja akiwa na vichwa viwili.

Hayo ndio yaliyojiri Alhamisi ya jana tarehe 18 July 2013 Huku katika Jimbo la Irolini Kwara, Nigeria. Hata hivyo mbuzi huyo alizaliwa na vichwa viwili alifariki saa chache baadae

Friday, July 19, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA PROFESA LIPUMBA KWA MAZUNGUMZO IKULU DAR


  
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alikutana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam.
 
 Mazungumzo hayo yalihusu masuala mbalimbali ya siasa na uchumi nchini.Pichani Rais Kikwete akiwa na Professa Lipumba katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana. 
 
Rais Kikwete, akiagana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba baada ya mazungumzo yao jana. Picha na Fredy Maro

MNYIKA AANIKA NAMBA ZA MAWAZIRI KWA UMMA...!!!

  Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.

Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba kwamba; “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:

Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.

Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

WEMA SEPETU KUOZEA JELA, ALICHOKIFANYA SAFARI HII....!!!


KUNA kila dalili kwamba mrembo anayetamba kwenye filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au Madam jela inamwita na anatakiwa kufanya maombi ili kukwepa kifungo maishani mwake.

Hali hiyo inafuatia staa huyo kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena Jumatano iliyopita, pale alipopanda katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar kwa kosa la kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni meneja wa hoteli moja iliyopo Kawe Beach jijini Dar, Godluck Kayumbu.


Kabla ya  kupandishwa  kwa ‘pilato’,  staa huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame alikuwa akisakwa na askari kwa siku kadhaa na kufanikiwa kuwapiga chenga za hapa na pale.

ANASWA AKIFUTURU
Hata hivyo, mbio zake ziliishia ukingoni Julai 16, mwaka huu, alipokamatwa saa mbili usiku akiwa anafuturu na wageni wake nyumbani kwake, Kijitonyama Dar.

MTITI KIDOGO
Askari saba walifika nyumbani kwake wakiwa ndani ya Land Rover ‘difenda’ kwa ajili ya kumkamata, hata hivyo walipata upinzani kidogo kutoka kwa mlinzi wa staa huyo ambaye alikuwa akizuia bosi wake asikamatwe ambapo ilibidi askari hao wakaze msuli na kutuliza mtiti uliokuwa ukitaka kutokea.

MZEE WA MIAKA 63 ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMBAKA MSICHANA WA MIAKA 16 NDANI YA MSIKITI...!!!


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma, imemhukumu Ahamad Fadhil (63), kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 ndani ya Msikiti wa ni Mwembe Mmoja, mjini hapa.

Hukumu hiyo ilitolewa na jana na Hakimu wa mahakama hiyo, Obadiah Bwegoge, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa.


Hakimu Bwegoge alisema mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili liwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.


  Alisema upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo mashahidi watano ambao bila kuacha shaka, walithibitisha kuwa mshtakiwa huyo alimbaka msichana huyo (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.


Alisema shahidi wa kwanza upande wa Jamhuri ambaye ni mlalamikaji, alidai kuwa siku ya tukio, saa nane 8:00 mchana, alikwenda msikitini hapo kuomba msaada kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kifafa.

SERIKALI YASISITIZA KUWA "KODI YA LINE ZA SIMU" IKO PALE PALE...!!!


Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesisitiza uamuzi wa Serikali kuendelea kutoza Sh 1,000 kwa kila mwezi kwa laini ya simu, licha ya kampuni za simu na wanasiasa kupinga.

Akizungumza na mwandishi juzi, Mgimwa alikumbusha wanaolalamikia kodi hiyo, kwamba suala la ulipaji kodi kwa taasisi au watu binafsi, ni la kisheria kulingana na mapato yao na hali halisi iliyopo.

Pia alieleza kushangazwa na matangazo ya baadhi ya kampuni kuhusu utozwaji kodi wananchi akisema wananchi ndio wanataka barabara, maji na umeme vijijini na kodi hizo zinakwenda kutumika huko.

Kwa mujibu wa Mgimwa, kodi ya laini za simu na ya intaneti, imetengwa ikatumike kusaidia maji na uwezo wa Serikali kupeleka elimu vijijini jambo ambalo ni la maendeleo.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 19, 2013

MASISTER BANDIA WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA ...!!!

Wanawake watatu wamekamatwa kwa madai ya kujaribu kusafirisha dawa za kulevya kupitia uwanja wa ndege wakiwa wamevalia kama masista.
 
Wasafirishaji hao walisimamishwa wakati wakiwasili kwenye kituo maarufu cha mapumziko nchini Colombia, sababu polisi walifikiri kwamba mavazi yao hayakuwa yakionekana halisia.
Maofisa waligundua kwamba kila mwanamke kati yao alikuwa na zaidi ya kilo 4 za cocaine zikiwa zimefungwa katika miguu yake.

Wakiwaongezea fedheha katika mashitaka, wasafirishaji hao walipangwa mstari mbele ya waandishi wakiwa bado wamevalia mavazi yao ya kituko kuficha ukweli.

LOWASSA AMCHAMBUA RAIS KIKWETE...!!!


Na Swahili TV
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa  Edward Lowassa, amemsifia Rais  Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshima  katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.

“Ni hivi karibuni  tu  Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani  George W.Bush  walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa Lowassa.

TAARIFA MAALUM YA TFDA KWA UMMA KUHUSU UTHABITII WA DAWA AINA YA 'DICLOFENAC' ILIYODAIWA KUWA NA MDHARA MWILINI..!

1.Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ina jukumu la kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakiki ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

2. Hivi karibuni, TFDA imepokea taarifa ya kuwepo kwa hofu juu ya usalama wa dawa aina ya Diclofenac kupitia mitandao ya simu na vyombo vya habari. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:
a. Diclofenac ni dawa iliyoko kwenye kundi la dawa zinazojulikana kitaalam kama “Non – Steroidal Anti-inflammatory Drugs”(NSAIDs). Dawa hizi hutumika kutuliza maumivu na kuondoa uvimbe unaosababishwa na



magonjwa mbalimbali. Magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya viungo, mifupa, uvimbe wa fizi na maumivu ya kichwa.

b. Mamlaka imesajili dawa ya Diclofenac kutoka makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi baada ya kutathmini ubora, usalama na ufanisi wake. Hata hivyo Diclofenac, kama ilivyo kwa dawa nyingine, ina madhara yanayofahamika. Kwa baadhi ya wagonjwa Diclofenac inaweza kusababisha vidonda vya tumbo, kuumwa kichwa, kuharisha, kutapika na kuwashwa mwili.



c. Pamoja na madhara yaliyoainishwa hapo juu, hivi karibuni imetolewa taarifa na Mamlaka ya udhibiti wa dawa ya nchi za Umoja wa Ulaya (European Medicines Agency) kwamba watu wenye matatizo ya moyo na shinikizo la damu, kisukari, waliowahi kupata kiharusi, wenye lehemu (cholesterol) nyingi kwenye damu, mshituko wa moyo na wanaovuta sigara wanaweza kupata matatizo kwenye moyo na mfumo wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.

Thursday, July 18, 2013

HUYU NDIYE STAA WA FILAMU BONGO ANUSURIKA KUFA KATIKA AJALI YA GARI...!!!

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel amesema amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari hivi karibuni.

Akizungumza na mwandishi wetu, Jacqueline alisema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbezi alipokuwa akielekea nyumbani kwa mama yake, Mbezi jijini Dar akiwa kwenye gari lake dogo, aliligonga kwa nyuma gari aina ya DCM.

“Ni ajali ya ajabu kweli niliipata, maana DCM limefunga breki za ghafla mbele yangu na mimi nilikuwa nimejisahau nikalivaa ila namshukuru Mungu kwa kuwa sijaumia ila gari langu tu ndiyo limeharibika vibaya kwenye shoo ya mbele,” alisema Jacqueline.

WASTARA JUMA "NAHITAJI MUME NA SI MWANAUME WA KUPITA"

 
 
STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma amesema hana haraka ya kuolewa kwani anahitaji mume na si mwanaume  wa kupita

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Wastara alisema kwa sasa yupo huru kutoka na mtu yeyote ampendaye kutokana na sheria na dini inavyosema ila kwa sasa shughuli za kuigiza zimembana.
 
‘Nahitaji mume na si mwanaume  wa kupita,  awe mvumilivu, mchapakazi pia awe na hofu ya Mungu. Kwa sasa nafanya filamu zangu kama kumuenzi marehemu mume wangu,” alisema Wastara. 
Na GPL

UJUE UKWELI WA DAWA ZA KULEVYA WALIZOKAMATWA NAZO MASOGANGE NA MWENZAKE, ADHABU YAO MIAKA 20 AU KIFUNGO CHA MAISHA


 
 Mellis Edward kushoto na Agness Masogange kulia waliokamatwa  na madawa ya kulevya nchini Afrika kusini
****
BAADA ya kukamatwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, ukweli umeibainika kwamba dawa walizokamatwa nazo ni za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazipatikani nchini na hazina matumizi yoyote.
Kupitia taarifa rasmi zilionesha kuwa, Chemical bashirifu ndiyo aina ya dawa walizokamatwa nazo nchini humo, ambapo wasanii hao walikamatwa nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam leo Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Kuthibiti Dawa za Kulevya nchini, Christopher Shekiondo alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za nchi, dawa walizo kamatwanazo wasichana hao zinatumika kutengenezea dawa za kulevya, ambapo adhabu yao ni sawa na mtu aliyekamatwa na dawa za kulevya.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JULAI 18, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...