Saturday, July 20, 2013

KOCHA MZUNGU TAIFA STARS AFARIKI DUNIA JANA

Bert Trautmann

 
Tumempoteza: Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Bert Trautmann amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89 jana.


Na Mahmoud Zubeiry na Chris Wheeler,
KOCHA wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na giwji wa zamani wa klabu ya Manchester City, Mjerumani Bert Trautmann amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 89.
Baada ya BIN ZUBEIRY kusoma taarifa za kifo cha kocha huyo Daily Mail, ilimpigia Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Leodegar Chilla Tenga ambaye alifundishwa na Mjerumani huyo na akasikitisha.
Tenga, ambaye sasa ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alisema kwamba Trautmann, ambaye alikuwa anasumbuliwa alikuwa mwalimu mzuri na wachezaji walimpenda sana.
Alisema kocha huyo aliyefariki asubuhi ya leo nyumbani kwake, La Losa, karibu na Valencia aliifundisha Taifa Stars kati ya mwaka 1975 na 1976.
“Alikuwa kocha mzuri, kwa sababu ni kocha aliyetokea kuwa mchezaji wa kulipwa, alikuwa anaelewa saikolojia ya wachezaji, na alikuwa mwalimu ambaye ukienda kambini unaona raha kuwa kambini.
“Alikuwa anatoa mazoezi magumu, lakini falsafa yake ilikuwa ni kumfanya mchezaji ajue majukumu yake na aweze kujitunza. Zamani sisi, siku za wikiendi tulikuwa tunabanwa, lakini alipokuja yeye baada ya mazoezi asubuhi, alikuwa anaturuhusu na kutuambia tukutane siku inayofuata muda wa mazoezi.
“Alikuwa anaangalia nidhamu ya mazoezi. Aliwapa uhuru wachezaji, kwa sababu alikuwa anaamini mchezaji siyo mtoto wa shule, ukimpa majukumu anayatekeleza. Ila mtu asipozingatia nidhamu ya mazoezi, kwake alikuwa hana nafasi tena,”.
“Kwa kweli tulimpenda sana, hakuna mchezaji ambaye alifundishwa na Bert hakufurahi kufundishwa naye. Mungu amuweke pema poponi,”alisema Tenga.
Bert alikuwa akifanya kazi na mzalendo marehemu Ray Gama kama Msaidizi wake, na baada yake kocha wa kigeni aliyemfuatia ni Mpoland, Vladimir Work ambaye alikwenda na Taifa Stars kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Nigeria.
Mfungwa huyo wa zamani nwa kivita Ujerumani Uingereza anakumbukwa kwa kuiwezesha City kutwaa Kombe la FA mwaka 1956 licha ya kucheza kwa dakika 17 za mwisho akiwa amevunjika shingo.
Mke wa Trautmann amethibitisha kifo cha mumewe kwa Chama cha SOka Ujerumani na Rais wake, Wolfgang Niersbach amesema: "Bert Trautmann alikuwa mwanamichezo mkubwa na Mjerumani halisi. Alikuja kama askari England na alikuwa shujaa. tayari alikuwa gwiji aliye hai. Maisha yake yatabakia kuwa kwenye vitabu vya histroria.’
Trautmann alikuwa mwanachama wa Hitler Youth na askari aliyepigana vita Kuu ya Pili ya dunia.
Alichezea klabu ya St Helens Town kabla ya kusajiliwa City mwaka 1949, lakini uamuzi wa utata wa klabu kumsajili kipa huyo Mjerumani ulisababisha watu 20,000 waandamane.
Bert Trautmann

Gwiji wa City: Alizaliwa Ujerumani, Trautmann akaichezea zaidi ya mechi 500 klabu ya Manchester

Pamoja na hayo, Trautmann akawateka mashabiki baada ya kuthibitisha yeye ni mmoja wa makipa bora wa kizazi chake, akiweka rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mkwa 1956.
Trautmann anafariki akiacha historia kubwa enzi zake baada ya mwaka 1956 katika Fainali ya Kombe la FA kuvunjika shingo wakati akichupia mpira miguuni mwa mshambuliaji wa Birmingham City, Peter Murphy.
Lakini aliendelea kucheza na kuokoa michomo kadhaa hadi akaiwezesha City kushinda 3-1.
Bert Trautmann

Trautmann alicheza kwa dakika 17 Fainali ya Kombe la FA mwaka 1956 licha ya kuvunjika shingo
Bert Trautmann

Baada ya Fainali hiyo ndipo vipimo vya X-ray vilipoonyesha Trautmann amevunjika shingo

Taarifa ya Manchester City imesema: "Bert Trautmann, mmoja wa makipa wakubwa Manchester City kwa muda wote na gwiji wa kweli wa klabu, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89, mwanawe wa kiume amethibitisha leo,".
Bert Trautmann
Mmoja wa walio bora: Lev Yashin, anayepewa heshima na wengi kama kipa bora zaidi daima kuwahi kutokea, amesema Trautmann alikuwa kiwango cha dunia
Bert Trautmann
Aliichezea zaidi ya mechi 500 City na kisha akafanya kazi ya ukocha kwa muda mfupi kabla ya kupewa kazi na Chama cha Soka Ujerumani ya kwenda kuprompoti soka katika nchi kama Burma, Tanzania na Pakistan.
Trautmann alistaafu mwaka 1988 na kwenda kupumzika nyumbani kwake Hispania na mkewe Marlis. Mwaka 2004 alipewa tuzo ya heshima ya OBE

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...