MAAJABU:MBUZI AZALIWA NA VICHWA VIWILI TENA KWA MAUMIVU MAKALI
Kuanzia Saa 10 Alfajiri zilisikika kelele za Maumivu kutoka kwa mbuzi
jike ambaye alikuwa anajifungua, Kelele zilikuwa kubwa mno kuashiria
maumivu makali alikuwa anayapata kiumbe huyo, palipozidi kupambazuka
ilibidi majirani waende kushuhudia kulikoni kwa mbuzi kuwa na kelele
kiasi kile, na ndipo walipojionea maajabu baada ya mbuzi jike huyo
kujifungua watoto watatu, wawili kati ya hao wakiwa ni wa kawaida kabisa
na mmoja akiwa na vichwa viwili.
Hayo ndio yaliyojiri Alhamisi ya jana tarehe 18 July 2013 Huku katika
Jimbo la Irolini Kwara, Nigeria. Hata hivyo mbuzi huyo alizaliwa na
vichwa viwili alifariki saa chache baadae
No comments:
Post a Comment